PICHA: Muinjilisti Daudi Mashimo akiwaombea baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuongea nao. |
Katika hatua ya
kuwaombea waandishi pia aligusia utendaji mgumu wanaopitia waandishi ikiwa ni
pamoja kutopewa mikataba au ujira kutokana na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya
habari kujikusanyia wao mapato huku waandishi wakisahaulika wakati wao ndiyo
wanaosababisha upatikanaji wa hizo habari.
Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Yesu kristo alipatwa
kuulizwa na wayahudi je, ni halali kulipa kodi? Jibu lilikuja kutokakana na
mazingira ambayo yalipelekea kuonekana ni halali kulipa kodi, maana hata yeye alilipa
kodi ya bwana kaisari kwa wakati huo. Ukisoma kwenye msaafu wa Biblia Warumi
13:1-8 inaeleza juu ya ulipaji wa kodi, hiyo inaonekana leo katika maisha ya wananchi
wa nchi mbalimbali wanaolipa kodi.
Kodi ndiyo moyo wa
taifa lolote linaloendesha serikali iliyo madarakani kuwatumikia wananchi ili
kufikia malengo kwenye huduma mbalimbali za kijamii ikiwa na kulipa mishahara ya
watendaji pamoja na kununua bidhaa muhimu kama madawa kwa ajili ya hospitali nk.
Wakati Rais John Pombe
Magufuri akikaribia kutimiza mwaka mmoja toka alipochaguliwa kuwa Rais,
kumekuwepo na watu mbalimbali wanaotoa matamko yenye lengo la kusifu na kuonyesha
utendaji mzuri au kumtia nguvu kuwa afanye nini ili afikie mafanikio zaidi.
Kama anavyojiita; Mchungaji
wa manabii nchini, muinjilisti Daudi Mashimo kutoka Calvary church amejitokeza
na kuiomba serikali ya Rais Magufuli kufuta msamaha wa kodi kwa mashirika na
madhehebu ya dini kutokana na kuwa hayana manufaa kwa wananchi, ikiwa ni pamoja
na kuwa yanapata faida kubwa kutoka kwenye biashara wanazofanya zisizolipiwa
kodi.
Muinjilisti mashimo
amekwenda mbali zaidi na kusema ikiwa mashirika na madhehebu ya dini nchini
yanamiliki mashule, mahospitali na biashara nyingine nyingi, akitolea mfano wa
shule za taasisi za dini, “mashule yao yanatoza ada
kubwa kwa wanafunzi wanaosoma kwenye hizo shule ambazo hazilipi kodi wala
kulipa ushuru kwa malighafi zinazojengea shule, lakini ndizo zenye bei/ada ya
juu kuliko baadhi ya shule zinazolipa kodi na ushuru kwa malighafi za kujengea
shule” alisema.
Pamoja na kumuomba Mh.
Rais Magufuli kuwa taasisi hizo zilipe kodi, anaelezea ni namna gani baadhi ya
watu kwenye madhehebu hayo wanavyofaidika na kutolipwa kwa kodi huku wananchi
walio wengi wanaumia na kukandamizwa kutokana na kulipa ada na huduma nyingine
kama kwenye hospitali za taasisi hizo.
Hata hivyo anasema “naimba serikali kurudisha kodi ya kichwa, maana vijana
wengi hawafanyi kazi wakijua serikali haitawabana hivyo kurudishwa kwa kodi hii
itawafanya vijana kuwajibikwa wakijua wana cha kulipa kila baada ya muda flani
na serikali isipotii hili, nitaendelea kumuomba Mungu anipe nguvu kulisimamia
hili.”
Akitaja 1Samweli 8:1-15
ambayo inaonyesha jinsi watu viongozi walioaminiwa kupewa nafasi ya kuongoza
baadaye wanapokea rushwa na kukacha madaraka, mwishowe wanahusiwa juu ya kodi. Muinjilisti
Mashimo analibainisha.
Post a Comment