TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Makamu wa Rais mama
Samia Suruhu Hassan ametunuku Tuzo makampuni 50 yanayofanya vizuri katika kusambaza
na kuhamasisha watanzania kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini.
Katika hafla hiyo iliyobeba
kampeni ya FAHARI YA TANZANIA ina lengo la kuhamisisha watanzania kutumia
bidhaa za nchini zilizokidhi ubora, kuongeza thamani, utoaji wa huduma, kukidhi
matakwa ya soko, ufanisi, ushindani katika soko pia inalenga mauzo ya bidhaa za
ndani kuteka soko la bidhaa za nje ya nchi badala ya watanzania kujivunia vya nje
ya nchi basi wanapaswa kujivunia bidhaa za zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
PICHA: Mkurugenzi wa tpfs Godfrey Simbeye akiongea katika uzinduzi wa Fahari ya Tanzania. |
PICHA: Makamu wa Rais Samia Suruhu akizindua nembo itakayotumika kuonyesha na kuthibisha bidhaa Fahari Tanzania, pembeni ni mkurugenzi wa TPFS Godrey Simbeye. |
PICHA: Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage akizindua nembo, akiwa pamoja na viongozi waandamizi na waandaaji wa FAHARI YA TANZANIA. |
Mkurugenzi mtendaji wa
tpsf Godfrey Simbeye amebainisha jinsi taasisi hiyo inayoshirikiana na wadau
wengine katika sekta ya viwanda wakiwemo tbs kuwa, wajasiliamali nchini
wanapaswa kutumia na kutunza utendaji ikiwa ni pamoja na kukuza uzalishaji wa
bidhaa ili kufikia viwango.
Dira ya taifa ya
maendeleo inaipa nafasi sekta binafsi kwenye uzalishaji ili kuchangia maendeleo
ya kijamii na pato la taifa, anasema uchumi utakuwa mpaka kufikia 7.9 kwa mwaka
huu, huku Tanzania ikiongoza kwa watalii wengi kuja nchini hii ni kutokana na
sekta binafsi zikishiriki kukuza na kutangaza utalii nje ya nchi.
Waziri wa viwanda,
biashara na uwekezaji Charles Mwijage (MB) anasema pamoja na wazo la
kushindanisha uwezo wa viwanda vyetu vya ndani, sekta binafsi na wazilishaji
nchini lilitokana na tbs na tpsf serikali inanafasi kuongeza ubia ili kuonyesha
mwanga kwa wazalishaji na kuwapa nguvu itakayoweza kuwanya watanzania wajivunie
bidhaa za hapa nchini
Makamu wa Rais mama
Samia Suruhu Hassan ambaye alikuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo huo,
anafarijika kwa ushirikiano unafanywa kati ya taasisi binafsi na taasisi za
serikali ambayo ni hatua nzuri katika kuleta maendeleo ya kweli katika taifa,
ikiwa ni utekelezaji wa sera na sheria ya Ushirikishwaji wa Umma katika Sekta
Binafsi (Public Private Partnership -PPP)
“natoa wito
kwa Taasisi ya sekta binafsi na wadau wote kuifanya kampeni hii kwa bidi na
nguvu zenu zote kwa kutoa elimu kwa watanzania wote kuwaeleza kwa kina umuhimu
kwa wao kununua bidhaa au huduma zinazozalishwa nchini na kuwakumbusha kuwa
kila mara wanaponunua bidhaa kutoka nje moja kwa moja wanatoa ajira kwa vijana,
wakulima na wawekezaji wa viwanda kwa nchi ambayo ile bidhaa imezalishwa na
kuongeza uchumi wa nchi hiyo, wakati kwa upande mwingine wanawakosesha ajira
vijana wetu, soko la mazao ya kilimo na kuendelea kudumaza uchumi wetu na kuwa
tegemezi” alisema
Makamu wa Rais Samia Suruhu Hassan.
Pamoja na hilo ameagiza
wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji ikiwa na pamoja na taasisi zake
kushirikiana kwa karibu zaidi na taasisi ya sekta binafsi tpsf pamoja na wadau
mbalimbali katika kufanikisha kampeni ya watanzania kujivunia cha kwao “Fahari ya Tanzania” huku wananchi
wakitakiwa kutumia fulsa hii kutumia bidhaa na huduma zetu ndani nan je nchi.
Post a Comment