0
PICHA: Afisa Mipango, Uchumi na Utawala wa umoja wa Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika mashariki Rodrigo Romero van cutsem akiongea na wadau kutoka  sekta mbalimbali kuhusu mipango ya uchumi inavyoweza kukuza uchumi katika nchi jumuiya za Africa mashariki.


PICHA: Wadau wa sekta binafsi wakisikiliza kabla ya kujadiri kutoka kwa Afisa Mipango, Uchumi na Utawala wa umoja wa Ulaya (EU) kwa Tanzania na Afrika mashariki Rodrigo Romero van cutsem (hayupo pichani) kuhusiana na masuala ya biashara kutoka nje ya jumuiya ya ulaya zinavyoleta nafasi kwa watumiaji wa ulaya kufanya uchaguzi kulinganisha na bidhaa za ulaya.


PICHA: Wadau wa sekta binafsi kutoka mashirika mbalimbali nchini na nje ya nchi wakimsikiliza afisa mipango, uchumi na utawala wa umoja wa ulaya kwa Tanzania na Afrika mashariki Rodrigo Romero van cutsem (hayupo pichani) masuala ya biashara kutoka nje ya jumuiya ya ulaya zinavyoleta nafasi kwa watumiaji wa ulaya kufanya uchaguzi kulinganisha na bidhaa za ulaya.




PICHA: Mkurugenzi mtendaji wa TPSF ndg Godfrey Simbeye akiongea na vyombo vya habari juu ya nasafi ya sekta binafsi katika kukuza uchumi.

Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Wadau mbalimbali wa sekta binafsi na masuala ya uchumi wamekutana ikiwa ni katika jitihada ya kujifunza njia mbalimbali zitakazowezesha kutimiza kwa mafanikio sera na mikakati inayotegemea ufanisi, uimara na ushindani uliopo katika upande huo.

Katika majadiliano hayo yaliyojumuisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi na jumuiya za kimataifa, yamelenga mikataba kadhaa ikiwemo mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na ile ya Umoja wa Ulaya (EU) umelenga kujadili, kufanikisha malengo yaliyopo ambayo ni pamoja na kuwawezesha watanzania na wanajuiya ya Afrika mashariki kufumbua macho na kuangalia fulsa kama ni nzuri na zinaweza kuwa na manufaa.

“mwaka 2012 tuliangalia kama kuna maslahi yoyote yanayoweza kupatikana endapo sekta binafsi inaweza kupata japo serikali ilitoa nafasi kujadili, kuzungumza na kuchukua fulsa zinazopatikana ikiwa ni pamoja na kutumia nafasi iliyotolewa na Rais John P. Magufuri kwa sekta binafsi kutumia fulsa katika kuendeleza nchi” anasema Salum Shamte Makamu mwenyekiti wa TPSF.



Post a Comment

 
Top