PICHA: Makamu Rais Samia Suruhu akifungua kongamano la wataalamu watafiti mbalimbali wa magonjwa nchi katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl. Nyerere jijini Dar Es Salaam. |
PICHA: Wataalam wakisikiliza kile kinachoendelea katika kongamano la utafiti na lililo hudhuliwa na naibu waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla, wa pili kutoka kushoto na Makamu wa Rais Samia Suruhu katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl. Nyerere jijini Dar Es Salaam. |
Leonard Mutani.
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Nchi ikiwa katika
maendeleo ya viwanda, wataalam wa afya nchini wameazimia kufikia maendeleo
endelevu yatakayowafikisha katika maendeleo ya afya itakayonyanyua wigo wa
huduma za afya hapa nchini.
Akifungua kongamano hilo
la kitaifa linaloudhuliwa na wataalam wa Afya kutoka taasisi mbalimbali makamu wa
Rais Mama Samia Suruhu ametanabaisha mambo mbalimbali akigusia hatua mojawapo
ya sekta binafsi zinazoudhulia kongamano hilo waweze kufanya jitihada kunyanyua
uwezo wao katika utafiti anasema “utafiti kwa taasisi zetu unatakiwa kuwa wenye
ubunifu wenye mbinu kubwa na za kisasa"
Vilevile utafiti
unaofanywa hapa nchini uwe na uwezo utakao wasaidia wananchi na nafasi hiyo itumike
ipasavyo kwa taasisi na sekta zinazohudhulia kongamano hilo la 30, ambalo
limeudhuliwa na baadhi ya wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani,
Australia na nyinginezo, hata hivyo
Makamu wa Rais aliongeza kwa kusema; “…serikali itaendelea kusaidia ubunifu,
maendeleo katika sayansi na teknolojia ya kuongeza kasi ya utafiti katika kuboresha
afya na mipango inayoweza kuruhusu watafiti kupendekeza ubunifu wa miradi kwa
upana. (Biomedical)
|
Post a Comment