PHOTO: Moto unaotokana na uchimbaji wa gesi kwenye mgodi. |
Sera ya taifa ya utekelezaji
wa mpango mkuu wa nishati ya gesi asilia
wa mwaka 2015 inahainisha matumizi ya rasilimali, kuboresha miundo mbinu,
maendeleo katika maeneo ya miji nchini.
Gesi iliyogunduliwa
nchini itaweza kuondoa au kupunguza matumizi ya mkaa na kutoka kwenye uharibifu
wa mazingira ambapo matumizi hayo ya gesi yataenda sambamba katika upatikanaji
wake hasa vijijini, ukizingatia tatizo linalofanya kukatwa kwa miti ni bei na
upatikanaji.
PHOTO: Naibu katibu mkuu wizara ya nishati na madini Prof. James Mdoe mwenye miwani, Kulia kwake ni Eng Innocent G. Luoga wakiongea na wanahabari. |
“Ni malengo
yetu kama taifa kuwa licha ya changamoto iliyopo kwenye upatikanaji wa gesi
baharini, lakini bado tutakuwa na uwezo utakaofanya matumizi ya gesi hii lazima
uzingatie matumizim ya ndani nchini kabla ya kusambaza nje ya nchi ili kuweza
kuwapa faida wananchi na kuona matunda yake.” Amesema naibu katibu
mkuu wizara ya nishati na madini inayoshugulikia madini Pro. James Mdoe.
Post a Comment