Watumiahi watatu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Seliani mkoani Arusha wameuawa kwa kukatwa katwa na mapanga na kisha kuchomwa moto na wananchi wilayani Chamwino mkoani Dodoma walipokuwa katika shughuli za utafiti wilayani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha hilo na akasema kuwa atatoa taarifa za tukio hilo baadaye.
Waliouwawa Dodoma watambuliwa kuwa ni Nicas Magazine (dereva), Teddy Lumanga na Faraji Mafuru, Mratibu wa Utafiti kituo hicho Dk C. Lyamchai aeleza.
Hata hivyo gari walilokuwa wanalitumia maofisa hao wa kilimo liliteketea kwa moto baada ya hasira za wananchi hao kuamua kuliteketeza kwa moto.
PICHA: Gari walilokuwa wakilitumia maofisa utafiti wa killimo waliouwawa. |
Post a Comment