PICHA: Vijana wadogo wa chekechekea ambao wanahitimu
masomo kwa hatua ya top class na kujiandaa kuingia darasa la kwanza.
|
PICHA: Vijana wa darasa la saba wanaohitimu masomo yao kwa hatua ya darasa la saba wakiwa makini kufuatilia kila kinachojili katika eneo la tukio madare jijini Dar Es Salaam. |
PICHA:Vijana
wadogo wa chekechekea kutoka shule za Atlas Ubungo wakiimba moja ya wimbo
unaovuta hisia kwa lugha ya kifaransa.
|
PICHA: Vijana wadogo wa darasa la nne wa shule ya Atlas wakicheza na kuimba wimbo wenye asili ya lugha ya kijaluo kutoka nchini kenya eneo la Kisumu. |
PICHA: Wakishangaa kile kinachofanyika katika jukwaa la kutolea burudani, vijana wadogo wa chekechea (TOP CLASS) wanaohitimu elimu hiyo na kujiandaa kuingia darasa la kwanza mwakani |
PICHA:
Muimbaji wa nyimbo za dansi nchini Makasi jr akiimba wimbo wa kumsifu na
kumtakiwa maisha ya heri ndugu Rugambwa na mkewe ambapo katika siku hii
walitimiza miaka kadhaa ya ndoa yao.
|
PICHA: Ndugu Benjamin Nkonya kutoka Tamosco akiongea
wakati wa mahari hayo.
|
PICHA:
Zana Rugambwa Mkurugenzi msaidizi wa Atlas kwanza kushoto, Sylivanus Rugambwa
Mkurugenzi shule za Atlas, wakiwasilisha salamu na shukurani.
|
PICHA: Wakitoa heshima kwa dakika moja kwa kumbukumbu ya miaka 17 kwa kifo cha hayati baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere, ni viongozi mbalimbali wa waliokuwepo katika mahari hayo |
PICHA:
Rogers Shemwelekwa Afisa elimu manispaa sekondari kinondoni akiongea nafasi ya jinsi wasomi wa vyuo wanavyoweza kushindwa kimaarifa na wanafunzi wa shule hiyo.
|
PICHA: Wakionyesha furaha mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao kama wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo kushoto ni Candy Clemence Amlima na kulia ni Lucy Elias Magashi |
HABARI KWA UNDANI:
Leonard
Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Kumekupo
na nia thabiti wazazi au walezi kupata nafasi ya kumpa mtoto elimu kwa ajili ya
mafanikio baadaye. Shule za Atlas zenye matawi yake wilaya ya Ubungo na
Kinondoni jijini Dar Es Salaam, imefanya sherehe kwa wazazi ikiwa ni pamoja na
mahafari ya darasa la saba na wale wadogo chekechea (TOP CLASS) wanaotarajia
kujiunga na darasa la kwanza mwakani.
Katika
risala iliyosomwa na vijana wa shule hizo wanasema; wakati huo hawakuwa na
majengo kama waliyo nayo sasa, walimu wasiozidi 10, viti kama vilivyopo sasa,
maji, vyakula, sehemu za kuchezea na hata vitabu, wanajivunia walimu wanaojua
nini wanachofanya hivyo wanawashukuru na kuwathamini na “Tunapeleka shukurani
zetu kwa mkurugenzi Rugambwa na Mkewe.”
Ni
takribani miaka 17 toka kifo cha hayati baba wa Taifa Mwl. JK. Nyerere afariki
dunia inakumbukwa kuwa Mwl alitenda mema, ni maneno ya mwalimu mkuu Justus
Kagya akielezea mafanikio katika mahafari hayo ya 6 kwa tawi la Ubungo na 11
kwa tawi la madare kwa shule za Atlas. Vilevile mafanikio yanayotokana na
takwimu kuonyesha ufanisi kupitia wanafunzi kufanya vizuri, ikiwa ni matarajio
ya kuingia kwenye kumi bora kitaifa kwa matokeo ya darasa la saba yanyotarajiwa
kutoka hivi karibuni.
Wadau
wa elimu kwa shule na vyuo visizo za serikali na zisizogarimiwa na serikali
Tamosco iliyoanza mwaka 1998 inalenga kwenye njozi ya kuona kila mtoto wa
mtanzania anapata elimu bora, ndg Benjamin Nkonya anasema “ingawa mafanikio
wanayopata ni kwa juhudi za wadau binafsi, bado matatizo kwa shule binafsi kama
kufutiwa usajili kutokana na kuwa na eneo dogo la shule ni tatizo, hali hii inapelekea
watoto kukosa haki ya kupata elimu hivyo upoteza muelekeo na wengine uingia
katika makundi mabaya mabaya na kuwa scorpion!.”
Akitoa
mfano wa tukio moja kwa wakaazi wa Peramiho anasema “wazazi walijitolea kufyatua
na kuchoma matofali kwa ajili ya kujengea shule na madarasa yalipokamilika
matokeo yake hawakupata usajili kutokana na kukosa 62milioni kwenye akaunti,
hii ni moja ya changamoto tunazokumbana nazo shule binafsi, ikiwemo kodi kubwa
na kubadirika badirika kwa mihura.”
“Shule ya Atlas kwa
elimu ya msingi tawi la ubungo iliasisiwa mwaka 8.8.2000 na miaka 10 baadaye
tawi la madare ilifuata huku tukiwa na sekondari, mashine maalum ya kusafisha
maji zaidi ya lita 50,000 ndani ya masaa 5, shule zetu zimepanda kimasomo mpaka kufika nafasi
10 kimkoa, kupitia shule hizi tumefanikiwa kutoa ajira za kudumu 430 na ajira
za muda mfupi 150 ambapo wajasiliamali kupitia huduma mbalimbali wanazotoa
katika shule zetu, tumeweza kutoa mikopo isiyo na riba kwa wafanyakazi wetu
huku tukiwa na matarajio ya kujenga nyumba za ibada kwa kila Imani na
tukitarajia Atlas kuwa kutuo cha vipaji nchini.”Anasema mkurugenzi wa
shule za Atlas Sylivanus Rugambwa, ifahamike kuwa sekta binafsi zina nafasi
katika kuongeza mapato serikalini anatoa wito kuwa uhuru, uwajibikaji kwa wafanyakazi
na ushirikiano ndiyo msingi wa mafanikio, aliongeza.
Kabla
ya kugawanywa na kuwa wilaya mbili za ubungo na kinondoni, tulikuwa na shule za
msingi 140 na sekondari 137, katika hatua yoyote ya elimu mwanafunzi anaweza
kufanya na kufaulu vizuri lakini asiwe na maarifa, ansema afisa elimu sekondari
wilaya ya kinondoni Rogers Shemweleka aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafari
hayo na anasisitiza tatizo lililopo kwa shule na vyuo vyetu nchini kuwa ni
shida sana, tunapeleka msomi chuo kikuu ambaye kiuwezo anapitwa na mtoto
anayesoma kwa mfano Atlas, hili ni tatizo ambalo tutalifanyia kazi mapema.
“kuwa na msomi ambaye
akuandaliwa vyema ndiyo shida inayolikumba taifa na watoto kwa hawa wanaotoka
hapa atlas utashangaa hawapatikani serikali, ukizingatia nchi ilikuwa
‘corruption’ rushwa na ndiyo maana Rais Magufuli anapambana sana na rushwa ili
kujenga taifa lenye maadili.” Anasema Rogers Shemweleka afisa elimu
kinondoni. Lakini mmeonyesha nguvu kuliko shule zenye umri mkubwa ambazo
hazifiki hata kumi bora hivyo kutokana na kile mnachofanya ni moja kati ya
ambacho atlas mnamuunga mkono mh Rais kwa kutoa elimu bora. Pale ambapo mtoto
anahudumiwa vyema basi kuna haja ya yule anaye muhudumia apewe pongezi kwa kazi
kubwa anayofanya.
Hata
hivyo anatoa wito kwa wanafunzi kushika sana elimu na kujilinda na jambo lolote
baya kutokana na umri wao ili kufikia malengo, maana wazazi wanatafuta fedha
kwa nguvu na kujinyima kwa ajili yao, pasipo wao kuelewa fedha hizo zinatoka
wapi.
Post a Comment