0
Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya Hellen Semi amefariki leo kwa ajali ya gari huko Chalinze mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa kuzuia huduma Dr. Neema Rusibamayila amefariki dunia kutokana na ajali ya gari barabarani leo asubuhi wakiwa njiani kuelekea Dodoma kuhudhuria mkutano wa RMOs huku Mkurugenzi wa huduma kwa umma Hellen Semi akifariki dunia.


Dr. Neema na dereva wake walikimbizwa hospitali kwa kutumia gari la wagonjwa kuelekea hospitali ya rufaa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.


Ajali ilitokea katika eneo la lugoba Chalinze, wakati dereva alipokuwa akiyapita magari mawili kwa mara moja, lakini dereva wa gari ya mbele alionyesha kutomruhusu kupita na kuongeza mwendo, ili kuepuka kugongana uso kwa uso dereva wa gari alilokuwemo Dr. Neema aliamua kutoka nje ya barabara, ndipo akaingia shimoni na gari kujibamiza.

PICHA: Gari walilokuwemo mkurugenzi msaidizi wa elimu ya Afya kwa umma Hellen Semi  na mkurugenzi wa huduma Dr. Neema Rusibamayila mara baada ya kupata ajali katika wneo la Chalinze mkoani Pwani.

Post a Comment

 
Top