Watanzania watakiwa kuliombea taifa na viongozi ikiwa ni njia ya kudumisha Amani, upendo na Umoja ulioasisiwa na viongozi waliotangulia.
Akiongea na wanahabari mapema leo jijini Dar Es Salaam, nabii Samson Rolinga wa kanisa la Omega Ministry la jijini Dar Es Salaam amewataka wananchi kuungana nae katika semina ya siku tatu ya kuiombea nchi na vijana kiujumla.
Nabii Rolinga ameongeza kuwa kupitia semina hiyo watu watafunguliwa na itakuwa njia sahihi ya kufanikiwa kimaisha hasa vijana waliokuwa wanakikosa ajira.
Semina hiyo itakayoanza tarehe oktoba 21 hadi 23 mwaka huu itafanyika katika ukumbi wa urafiki –Nyangumi ubungo jijini Dar Es Salaam.
Post a Comment