Profile PHOTO: Bandari ya
Dar ikionekana kuwa na shehena ya mizigo inayosubili kusafirishwa kwenda sehemu
mbalimbali ndani na nje ya nchi.
|
Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Chama cha wafanyabiashara wa DRC wanaanza kuweka
mikakati itakayowafanya kutumia bandari ya Dar Es Salaam kupitishia mizigo yao
ikiwa ni ishara itokanayo na mazungumzo ya Marais wawili wa Democratic Republic
of Congo Kabila na Tanzania Magufuri.
Hatua hiyo inakuja baada ya vikwazo kadhaa
vilivyokuwepo nchini Tanzania ikiwepo kupunguza wingi wa vituo vya ukaguzi na
kimoja cha vigwaza kwa wafanyabiashara waopeleka mizigo DRC. Rais wa chama cha
wafanyabiashara wa nchini congo ndugu
Sumaili K. Edward anasema; “Sasa tunaanza kutumia bandari ya Dar Es
Salaam kutokana na mafanikio tuliyoyaona kwa viongozi ‘wazazi’ wamefanya kazi
kubwa kuonyesha mafanikio baada ya kukutana na kuongea na kufikia makubaliano”.
Pamoja na hilo vituo vya kupimia uzito wa magari
(weight Bridge) ilikuwa ni tatizo kubwa kutokana na mizani mingi ilikuwa
inasababisha mizigo kutofika congo sababu ya uzito, hivyo kupunguzewa kwa vituo
hivyo na kubaki vitatu inaleta nafuu pia kwa magari yanayoelekea DRC.
Katika hatua nyingine, mwezi wa November 2016
wafanyabiashara hao watakuwa wanapitisha mizigo yao ikiwa ni pamoja kutumia
(Grace Period) nafuu ya kupitisha mizigo yao bure kwa muda wa mwezi moja, baada
ya Rais John Pombe Magufuri kutoa kauli ambayo ndg Sumaili anasema ni moja ya
mafanikio makubwa sana wanayojivunia.
Kuonana kwa viongozi wakuu wa nchi ya Tanzania na
DRC kumepelekea hauweni kwa wafanyabiashara hao kuhudumiwa kwa haraka kwenye
ofisi Bandari ya Dar Es Salaam, akitolea mfano wa jana(06.10.2016) mmoja wa
wafanyabiashra aliyeshugulikiwa kupata file kwa muda mfupi wa masaa mawili.
Akimtaja kwa jina moja tu ndugu Kimaro mfanyakazi wa
mamlaka ya Bandari Tanzania ambaye alishugulikia file hilo ikiwa ni tofauti na
miaka iliyopita ambapo hali ilikuwa ngumu kupata huduma kwa haraka kiasi hicho, hivyo aliona faraja kubwa na kuharakisha kwa wafanyabiashra wote wa kongo kuanza kupokea shehena zao hapa Tanzania.
Post a Comment