|
PICHA: Rais John Pombe Magufuri. |
Kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh.Nape Nnauye leo akiwa ndani ya uwanja wa Taifa kuangalia uharibifu uliofanyika ktk mechi ya Simba na Yanga, Nnauye anasema kuwa jana alipigiwa simu na Mh. Rais JPM na akawa amekasilishwa kwa kitendo kilichofanywa na mashabiki wa pande zote mbili, kun'golewa viti pamoja na mageti nane ya upande wa Simba na Yanga yamevunjwa na ndani upande wa Simba kuna viti karibu 1782 zimeharibiwa.
|
PICHA: Upande ambao mashabiki wa simba walikaa na kuvunja viti. |
Gharama ya kila kiti ni shilingi laki mbili, hivyo basi kwa jumla ya gharama ya viti vyote bila mageti yaliyoharibiwa ni karibu milioni 300. Mh Nape Nnauye anasema Rais amekasirika kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lakini kama serikali uamuzi tuliochukua ni kuzifungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakapotoa taarifa nyingine. Lakini pia serikali imeamua kuzuia mapato yote ya Simba na Yanga mpaka watakapothibitisha kulipa uharibifu wote uliofanywa na mashabiki wao.
|
PICHA: Uharibidu ulifanywa na mashabiki wa soka wa simba na yanga. |
Mh. Nape anasema wataenda mbele zaidi kwa kufunga camera uwanjani hapo ili waweze kunasa sura za mashabiki watakaokuwa wanafanya vitendo vya uharibifu ndani ya uwanja huo ambao ni moja ya viwanja vya kisasa katika ukanda huu wa Africa mashariki, lakini pia kuweza kujua chanzo kikubwa cha vurugu katika mechi ya jana yawezekana ilikuwa ni mambo mawili; kwanza ni mfumo wa kadi kufeli, kadi nyingi ambazo zilikuwa zinasema kadi si halali na wakati huohuo mtu katoka kununua kwenye kituo na watu halali na kadi nyingine zilitoa taarifa huna salio la kutosha.
Ilitokea mtu ukienda kwa polisi basi unaambulia kirungu au kofi kwa kudhaniwa ni ulaghai, hali hii ndio ilisababisha watu waanze kuvamia mageti kwa kuona hakuna namna. Kadi umekata na uwanjani usiingie, serikali imtazame upya mzabuni aliyepewa kazi ya kuuweka mfumo wa kielectroniki ambaye majaribio yake ilikuwa ni mechi kubwa ya Simba na Yanga, mfumo ulionyesha kuelemewa au kushindwa kutokana na mazingira yaliyokuwepo.
Post a Comment