Na.John Luhende
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Kituo cha uwekezaji kimesema hatua ya serikali kuhamishia makao makuu yake mkoani Dodoma kumefungua fursa nyingi za uwekezaji katika mikoa jirani hasa mkoani Morogoro ambao una eneo kubwa linalo faa kwa uwekezaji wa kilimo, na viwanda.
Akizungumza na waandishi wa habari kaimu mkurugenzi wa kituo hicho Clifford Tandari amesema kituo cha uwekezaji nchini kwa kushirikiana na mkoa wa Morogoro wame andaa mkutano Mkubwa wa kuhamasisha na kukuza uwekezaji na biashara mkoani huko mwishoni mwa mwezi huu.
Naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Steven Kebwe amesema mkoa huo umejaaliwa kuwa na fursa na mazingira mazuri ya uwekezaji,na lasili Mali nyingi ambazo bado hazija tumika ipasavyo na wakati umefika Sasa kwa wawekezaji kuchangamkia fursa hiyo.
Post a Comment