PICHA: Prof. Anna Tibaijuka akiwa na Tuzo aliyopokea nchini Marekani. |
Kwa mara nyingine tena
aliyewahi kuwa mwanamke wa kwanza kutoka ukanda wa Africa mashariki kushika
wadhifa mkubwa wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Professor Anna Tibaijuka
ameendelea kuonekana kimataifa mara baada ya kushinda tuzo kutokana na juhudi
zake katika maendeleo ya jamii nchini.
Tuzo hiyo ya “His Royal Highness
Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award for Sustainable Development” ambayo inatolewa kwa niaba ya jamii unayotoka na wale
unaofanya nao kazi, uliyoonyesha mchango wa moja kwa moja na haiendi kwa mtu
binafsi, tuzo hiyo ambayo mfadhili wake mkuu ni waziri mkuu wa Bahrain.
Utoaji wa tuzo hizo
ambazo sherehe zake zilifanyika katika viwanja vya makao makuu ya umoja wa
mataifa ‘New York Marekani mnamo tarehe 24.09.2016 uliudhuliwa na viongozi
mbalimbali dunuani kutoka nchi kadhaa, ambapo kwa Tanzania iliwakilishwa na
Balozi Maige pamoja mbunge wa viti maalum Anna Lupembe.
Hata hivyo pamoja na
utolewaji tuzo hiyo, iliambatana na fedha taslimu dollar 100,000 ambazo mama
Tibaijuka anasema; “sikuzichukua kutokana na yaliyonikuta hapa mapema, kwa
halisi ya nyumbani hatua utaratibu wa kupokea tuzo/fedha kama zawadi, kwa hiyo
naicha mezani nyie fanyeni mtakavyoona yafaa, maana hayo ndiyo matatizo ya
taifa letu, ndiyo maana nimekuja hapa mambo yote yawekwe bayana
yazungumzwe wenye nia nzuri, na wenye
nia ovu kila mtu acheze anavyoona inastahili" alisema mama Anna Tibaijuka.
Katika hatua ya
kuonyesha umakini kwa watoaji tuzo, mara nyingi wamekuwa wakufuatilia hatua kwa
hatua kwa yale yote unayoyafanya ukiwa katika eneo lako la kiutawala kama mama
Tibaijuka anavyobainisha kuwa, ‘watu hawa wamekuwa wakitufuatilia kazi tunazofanya, hata
wakati nipo muleba nikifanya kazi na wananchi’ hivyo basi ukiwa kama
kiongozi unapaswa kuwa karibu na jamii ili pale unapojikwaa utaonekana na pale
unafanya vyema utaonekana.
HABARI KATIKA PICHA:
PICHA: Prof. Anna Tibaijuka akiangalia moja ya bango lenye ujumbe wakumpongeza Uwanja wa ndege wa Mwl. JNIA mara baada ya kuwasili akitokea Marekani. |
PICHA: Prof. Anna Tibaijuka mwenye kitambaa cha njano begani akiwa na baadhi ya wanafunzi, ndugu jamaa na marafiki waliokuja kumpokea uwanja wa ndege JNIA. |
PICHA: Prof. Anna Tibaijuka akionyesha cheti kwa ambacho kinampa kumbukumbu kama mmoja wa waliotunukiwa Tuzo hiyo. |
KITABU KINACHOONYESHA MCHANGO ALIOUTOA DUNIANI KWA SEHEMU MBALIMBALI ALIZOPATA KUTEMBELEA IKIWA NI PAMOJA NA NCHINI TNZANIA IKIW ANI PAMOJA NA JIMBONI KWAKE MULEBA. |
Post a Comment