Kongamano
lenye lengo la kuinua uwezo linafanyika ikiwa ni la kwanza tokea shirika la ChangeTanania lilipoanza miaka mitatu iliyopita, pamoja na kongamano hilo
lenye lengo la kutathimini na kujadili mbinu za kiubunifu na kuweza kupambana
na changamoto zinazoikumba jamii hasa kwenye matumizi ya teknorojia.
Mwazilishi
(CEO) wa taasisi hiyo isiyo ya kiserikali Bi Maria Sarungi Tsehai anasema “tulianza kwa kupitia mtandao ‘hashtag’ ya
change Tanzania na kilichotokea ni kwamba tuliweza kupata watu wengi ambao
wamekuwa ni member kupitia facebook na followers kupitia twiter ambao huwa
tunajadiliana siku zote juu ya kubalisha hali ilivyo Tanzania na wananchi
wenyewe wapate kubadirika siyo wasubiri serikali au mpaka wapate wafadhiri”
PICHA: Baadhi ya vijana mbalimbali ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa ni mchango mkubwa katika mabadiriko kutokana na wao kuwa watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii nchini na kwingineko duniani.
PICHA: Wakati wadau mbalimbali walishiriki na kutoa maoni yao viongozi na wageni kutoka nchi tofauti duniani waliudhulia, ambapo mgeni rasmi alikuwa Dr. Jabir Bakari ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa shirika la E-Government, (hayupo pichani)
Hata
hata hivyo mmoja wa waongozaji/(Usher) katika mkutano huo ndugu John Kiangi
anasema pamoja na kuchanganua changamoto kuna kuonesha na kuangaza mambo
yanaofanywa na vijana kijasiliamali, uwezo binafsi kama wa kutengeneza mitandao
mbalimbali, biashara ya kwenye mitandao pia huduma za kijamii
Post a Comment