Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Shirika lisilo la kiserikali la Twaweza limetoa utafiti mpya unaoangazia tofauti kadhaa katika
nyanja mbalimbali za kisiasa na kiuchumi mojawapo ikiwa ni jinsi gani wanaweza
kutambua maana ya neno Dikteta hama nafasi ya vyama vya siasa kuungwa mkono
katika harakati ikiwa ni pamoja na maandamano.
Katika kongamano hilo lilioshirikisha baadhi ya
watendaji kutoka vyama kadhaa vya kisiasa vikiwemo Chama cha mapinduzi –CCM kilichowakilishwa
na Ole sendeka na ACT –Wazalendo kilichowakilishwa na Zuberi Zito Kabwe ambapo
kwa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendelo –Chadema wao hawakuweza kufika,
liliweza kuwa na hamasa kadhaa kutoka kwa wahudhuliaji waliofika kwenye ukumbi
wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar Es Salaam.
Vilevile pamoja na tafiti hiyo asilimia 32% ya walitoa
maoni wanasema ni Utawala wa kimabavu au utawala wa nguvu pia asilimia 34%
hawajui maana ya udikteta, 15% wanasema ni mtu mmoja mwenye nguvu zote ndiye
dikteta na 2% wanasema ni uongozi mbaya. Katika hatua nyingine wananchi
wanaosema nchi inaongozwa kidteta kwa sasa ilikuwa ni 11% wanasema ndiyo, 58%
wanasema hapana, 31% hawajui.
PICHA: Msemaji wa CCM Ole Sendeka akizungumza wakati wa kuchangia Kongamano. |
Hata hivyo muwakilishi wa chama cha mapinduzi CCM
ambaye ni msemaji wa chama hicho anakubaliana na utafiti huo ambao umejitika
katika mawazo ya wananchi kuwa upo sahihi, huku akiuunga mkono kwa asilimia 99,
japo kile ambacho Rais magufuri anachofanya ndicho kile ambacho wapinzani
walikuwa wanakipigia kelele; Ole Sendeka anasema “Aliyokuwa anafanya Rais kama
msimamizi wa nidhamu na utumishi kwa mujibu wa katiba, alikuwa anatekeleza
mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano, katika kipindi
hicho nyinyi nyote mnaishi katika nchi hii, mnajua mambo yalipokuwa yamefikia,
ukwepaji wa kodi uliokuwepo na ndiyo maana haishangazi kuona asilimia kubwa ya
wale wenye fedha ndiyo wanaokubali kuwa Rais huyu ni dikteta.
Pamoja na hayo kiongozi wa ACT Wazalendo nchini Zito
Kabwe aliweza kusema; "lakini leo hii kikwete angenunua ndege cash bila procurement process Ole sendeka asingekaa Bungeni, angeongoza hiyo vuta ya sheria ya manunuzi kutofuatwa, kwa sababu kama hushindanishi watu wenye ku_supply unajua bei, unajuaje ubora? For the first time jana Rais wa nchi anawaambia watanzania kwamba 'bei ni siri ya kibiashara' hii ni fedha yangu ya kodi inakuwaje ni siri ya kibiashara?"
PICHA: Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zito Kabwe akiongea na waandishi wa habari kwenye kongamano hilo.
|
Pamoja na hayo mbunge huyo wa kigoma alizungumzia nafasi kuhoji pale panapoonekana pana muelekeo wa kutofuata sheria, ili kutovunjwa kwa katiba ya nchi, huku akisisitiza haja ya kulinda Uhuru wa mawazo ikiwa na maana hata kabla mwaka haujaisha zaidi ya watanzania (12) wako mahakamani kwa sababu ya maoni yao kwenye mitandao ya kijamii.
Mkurugenzi mtendaji wa Twaweza ndugu Aidan Eyekuze "Katika hali isiyo ya kawaida utafiti huu umeibua matokeo ya kufikirisha juu ya miitizamo ya watanzania kuhusu siasa za mfumo wa utawala" hivyo basi watanzania wengi wanaunga mkono mfumo wa demokrasia wa vyama vingi na uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni.
PICHA: Mkurugenzi wa Twaweza ndg Aidan Eyekuze akiongea jambo katika kongamano. |
Hili ni jambo la kuzingatiwa kwa serikali kwa wakati huu huku idadi ya wananchi hawakubaliani na kauli inayosema Rais magufuri ni dikteta. wakati huohuo inaonyesha kwamba wananchi wanasema ili kulinda amani na kuchochea kasi kubwa zaidi ya maendeleo wanaweza kukubaliana na baadhi ya vizuizi kwenye haki za binadamu. lakini vitendo visivyo vya kidemokrasia vitavuka mipaka, utayari wao wa kuvikubali unaweza ukabadirika.
PICHA: Baadhi ya waudhuliaji wa kongamano lililoandaliwa na TWAWEZA wakifuatilia kupitia mtandao www.twaweza.org/sauti kuona maona na kila hatua ya kinachoendelea katika upatikanaji wa utafiti huo. mstari wa mbele katikati waliokaa ni Kiongozi wa ACT Wazalendo nchini Zuberi Zito Kabwe.
Post a Comment