0
Shirika la ndege la Rwanda, Rwandair, limepiga hatua katika ushindani wa biashara ya uchukuzi wa abilia kwa ndege katika ukanda wa Afrika mashariki na kati huku likilenga kusafirisha abiria zaidi ya laki 700 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017.

PICHA: Muundo wa ndani wa ndege aina ya Airbus A 300s unavyoonekana ndani kwa juu.


Ndege hizo aina ya Airbus A300s zimetengenezwa nchini ufaransa, zilizinduliwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kanombe, Kigali nchini Rwanda italiwezesha shirika hilo kukamata masoko ya Ulaya na hata katika bara la Asia.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Rwandair John Mirenge aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 244 pamoja na mizigo isiyozidi tani 1.0 ndiyo ya kwanza katika ukanda huu wa Africa mashariki na kati huku ikiwa na teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu.

Moja kati ndege mbili aina ya AIRBUS A 300s zilizonunuliwa na shirika la ndege la nchini Rwanda.
Alisema; "Ukiwa angani ndani ya ndege hii unaweza kupiga simu, kupata ujumbe wako wa simu, ujumbe wa barua pepe, ujumbe wa WhatsApp na mawasiliano mengine. Haya hayakuwepo katika ndege nyingine tulizo nazo, hata katika ukanda huu na kwingineko barani africa hakuna shirika lenye ndege yenye uwezo huu".

Muundo wa viti ulivyo kwa ndani.

Ndege hiyo iliyotengenezwa nchini Ufaransa, imenunuliwa kwa kitita cha dollar za marekani milioni 200, ambapo safari inayotegemewa kuwa mwishoni mwa wiki ijayo ya tarehe 8 october 2016 kuelekea mjini Dubai

Bw Mirenge, ameongeza kwa kusema safari za shirika la ndege la Rwandair zilikuwa zinapatinaka kwa nchi kadhaa za Afrika magharibi na kati na hivyo basi uwepo wa ndege hii sasa inakuja kuongeza nguvu ya kuvamia masoko ya Ulaya, Asia na kusini mwa Afrika kama Africa ya kusini.

Post a Comment

 
Top