Ali Mbonde Akionyesha mitungi ya gesi iliyotumika. |
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Wafanya biashara wa soko la samaki fery, zone namba 6 wanaiomba serikali kuzungumza na kampuni ya gesi ambayo inatoa
huduma kwao katika kuwajengea eneo salama na lenye ukubwa la kuweza kuhifadhi
mitungi ya gesi.
Hayo yamezungumzwa na
mwenyekiti msaidizi Ali Mbonde wa soko hilo ambaye anasema kuwa chumba kinacho
hifadhi mitungi yao sio salama kutokana na eneo kuwa dogo na kupelekea kuganda
kwa gesi hadi kutolewa nje ili iweze kuyeyuka na kuweza
kutumika ambapo hali hiyo ni ya hatari kwa afya za wafanya biashara, wateja na watalii
wanaokuja kutembelea soko hilo.
Aidha Mbonde
amebainisha kuwa, kupanda kwa gesi kutoka 70,000 hadi 85,000 imekuwa nichangamoto kwao kutokana na
matumizi ya kukaanga samaki pamoja na mafuta wanayo tumia kwa hivi sasa kuwa ni
bei juu.
Mitungi ya gesi iliyokaa kwa muda mrefu pasipo kubadirishwa katika soko la samaki feri jijini Dar Es Salaam. |
Hata hivyo amewataka wenye
makampuni ya gesi kuweza kuwapunguzia bei ili
waweze kutumia mtungi mmoja kwa mtu mmoja na si mtungi mmoja kwa
watu wawili kama ilivyo sasa hivi.
Baadhi ya wachuuzi wa samaki sokoni hapo wakiandaa samaki kwa ajili ya kukaangwa. |
Post a Comment