Leonard Mutani
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Katika kuhakikisha
suala la elimu ya usalama barabarani inazingatiwa jeshi la polisi nchini kikosi cha usalama
barabarani kinatarajia kufanya maadhimisho ya wiki nenda kwa usalama barabarani
nchini, itakayofanyika mwezi October mosi huko mkoani Geita.
Kamishina wa Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mohamed Mpinga |
Akizungumza na
waandishi wa habari mapema leo, kamishna msaidizi wa kikosi cha usalma
barabarani DCP Mohamed Mpinga amesema kuwa maadhimisho hayo yataenda sambamba
na kauli mbiu ya HATUTAKI AJAL, TUNATAKA KUISHI SALAMA, (No road crushes, we
want to live safely).
“Ongezeko la vyombo vya moto nchini kwa upande mmoja na
ule wa ongezeko la watumiaji wa barabara wa ngazi mbalimbali hauna budi
kutiliwa maanani, ili kuweza kuzuia ajali za barabarani” Alisema na kuongeza, ajali
nyingi barabarani zimekuwa zikichangiwa na wadau mbalimbali wa usalama
barabarani kutojua sheria pamoja nakutumia vyombo vya moto ambavyo ni vibovu,
hivyo kuathiri hali ya usalama barabarani.
Wakati huo huo kauli mbiu ya mwaka
huu inasisitiza kila mtuaji wa barabara kufaham wajibu wake katika kuhakikisha
usalama barabarani unazingatiwa, na anasisitiza kuwa suala la usalama
barabarani siyo kazi ya kundi moja tu, bali ni la kila mtu anapaswa kujiona ni
muhusika.
“Wanahabari ni miongoni mwa wahusika wa suala la usalama
barabarani kwani kupitia wao wana nafasi kubwa kuielemisha jamii na umma kwa
ujumla ili kusaidia jitihada mbalimbali katika kujenga utamaduni wa kuheshimu
sheria za uslama barabarani nchini” Kamishina Mpinga
aliongeza kuwa, wakati wa zoezi hilo jeshi la polisi kupitia kitengo cha uslama
barabarani litatoa elimu kwa wadau mbalimbali wa barabara pamoja na kufanya
ukaguzi wa vyombo vya moto ikiwemo magari, bajaj na pikipiki. Vilevile zoezi
hili litaendana na utoaji wa stika za usalama barabarani kwa vyombo
vitakavyothibitika kuwa na ubora wa kutembea barabarani.
Ambapo alivitaja
viwango vya ukaguzi wa magari na kuwekea stika itakuwa katika mifumo mitatu;
magari ya biashara yatatozwa shs 5000/-, wakati magari madogo ya binafsi shs
3000/-, pikipiki na bajaj shs 1000/-.
Hivyo anawataka
wananchi kupeleka vyombo vyao vya moto katika vituo vya polisi kikosi cha usalama
barabarani kitengo cha ukaguzi wa magari ili kuweza kukaguliwa na kuhakikiwa.
“Endapo katika ukaguzi wa chombo chochote kitabainika kuwa
ni kibovu, basi mmiliki anapaswa kukipeleka kwa ajili ya matengenezo, na kisha
kukaguliwa kwa mara ya pili na kubandikwa stika maalum.”
Wakati huo huo kampuni
ya mafuta ya Puma Enegy ambayo imekuwa ikiwekeza kwa muda mrefu upande wa
barabara, ambacho inaamini ni kipengere muhimu katika maendeleo ya Taifa,
vilevile usalama barabarani umeendelea kuwa changamaoto kubwa duniani hivi sasa.
Philippe Corsaletti
ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Puma Enegy nchini amesema “tukumbuke kwamba
kuwekeza katika usalama ni kujenga nguvu ya baaadaye katika nyanja zote za
uwekezaji imara na kujenga uchumi endelevu kwa watu wetu”
Post a Comment