PICHA:
Kutoka kushoto; Bi Adolphine Kateka, Tajiel Urioh, Dennis Mwendwa, January
Makamba Waziri na Msimamizi wa Mjadara Philippe Boncour kutoka ubalozi wa Ufaransa.
Ubalozi wa Ujerumani
pamoja na Ufaransa wafanya kongamano la wiki hali ya hewa kidiplomasia juu ya
tabia nchi ambapo kumekuwa na majadiliano kwa baadhi ya wataalam na watafiti wa
masuala ya mazingira kutoka sehemu mbalimbali nchini huku upande wa serikali
ikiwakilishwa na mh; January Makamba waziri ofisi ya waziri mkuu
anayeshugulikia mazingira.
Dennis Mwendwa
ambaye ni mtaalam wa vyama vya kiraia anasema matumizi ya nguvu za jua yanaenda
kushika klasi zaidi duniani kuliko nguvu zozote kutokana na garama zake kuwa za
chini dunianin mfano nchini Denmark imeonekana wananchi wengi ni watumiaji wa
malighafi hiyo, huku 78% ya wananchi wakiaminika kutumia umeme wa nguvu za jua.
Hata hivyo Mwenwa
alisema umeme unaopatikana kwa malighafi nyingine unaweza kuwa wa bei juu au
hata kama ukiunganishwa kwenye gridi ya taifa bado unaweza usikidhi mahitaji,
hivyo basi, uzalishaji wa umeme wa nguvu za jua unaweza kuwa msaada sababu
hauna garama za ziada za kuendeshea na endapo kutawekwa machine kubwa za kuzalisha
nishati inayohitajika.
Wakati huohuo Mwema
ameongeza Serikali inabidi iwezeke kwa kiasi kukubwa upande wa wanyama kama
Tembo kutokana na wanyama hao kuuwawa kwa kiasi kikubwa kuliko hata uzao wao
unaochukua miaka miwili na kwa upande wa majangiri wanaua kwa spidi kubwa
kuliko kawaida, hivyo uwekezaji unaohitajika hapo ni kuweza kupata fedha na
kulinda vivutio hivi.
Waziri January Makamba kwa niaba ya serikali ameweza kugusia upatikanaji
wa malighafi za umeme jua kuwa aziwezi kuwafikia wananchi walio wengi hata zikiwafikia
bado garama zake zitakuwa kubwa kuliko umeme wa Tanesco. Hata hivyo katika hatua nyingine Makamba
amegusia kilimo kuwa wao kama serikali wanajitahidi kuwa=ekeza katika sekta
hiyo ikiwa na maana wananchi walio wengi wamejikita katika kilimo na serikali
yenyewe inawekeza katika kilimo kama uti wa mgongo.
Tarjie Urioh
yeye ni mshindi wa tuzo ya hali ya hewa kupitia nyanja tofauti, anasema upande
wa utalii, uwekezaji bado haujafanyika vya kutosha hivyo kumekuwapo na kuiona
sekta hii ya utalii ikiingiza mapato lakini bado haijapewa nafasi yoyote wala
kupewa nafasi ya kuwezesha ikiwa na maana utangazaji wa vivutio vya kitalii
umekuwa mdogo.
PHOTO: Waziri katika ofisi ya waziri mkuu anayeshugulikia mazingira, Mh. January Makamba.
|
Post a Comment