0

Rais na mwenyekiti wa ccm JPM ametembelea makao makuu ya ofisi za gazeti kongwe la chama cha mapinduzi kwa kushitukiza mapema leo mtaa wa Lumumba jijini Dar Es Salaam na kisha aliweza kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa chombo hicho.

Katika mazungumzo hayo, wafanyakazi hao wa gazeti hilo linalomilikiwa na chama kikongwe ccm wamesema, ni miezi saba (7) sasa imepita hawajalipwa mishahara yao, kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti katika hali ya sintofaham pamoja na kutopelekwa kwa michango yao ya NSFF, kutotambuliwa kwa baadhi ya wafanyakazi katika ajira ikiwa ni pamoja na madwni ya muda mrefu wanayozidai taasisi za serikali.

Vilevile wamemuelezea Rais Magufuri kuwa Bodi na menejimenti ya kampuni inaypendesha vyombo vya habari vya chama, Radio Uhuru pamoja na gazeti la Uhuru imeahindwa kuendesha vyombo hivyo na wamemuomba mwenyekiti huyo wa ccm kuingilia kati kuweza kuvinusuru kutokana na ukata pamoja na madeni makubwa na biashara kushuka.

Mwenyekiti huyo wa ccm na Rais wa Tanzania alielekea ofisi hizo za gazeti la Uhuru akitokea ofisini kwake mtaa wa Lumumba makao makuu ya chama aliweza kuwajibu wafanyakazi kwa kumuagiza katibu mkuu wa ccm Abdulrahaman kinana kuhahalisha kuwa mishahara yote wanayodai wafanyakazi inayofikia shs 609milioni inalipwa ndani ya mwezi huu wa tisa, pia ameagiza kupatiwa orodha ya vyombo vyote vya serikali vonavyodaiwa na gazeti la uhuru na mzalendo.

Pia ameahidi kufanyia kazi malalamiko yao juu ya kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha gazeti pamoja na suala la menejimenti, hata hivyo Rais magufuri amewapongeza wafanyakazi hao kwa moyo wao richa ya kuwepo kwa changamoto nyingi lakini wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha vyombo hivyo vinatoa habari.

Post a Comment

 
Top