Misaada ni jambo la
kawaida kwa mtu au taifa lolote duniani hasa pale panapokuwepo na majanga ya
kibinadamu au hata yale yaliyosababishwa na binadamu moja kwa moja, na lengo la
msaada unaletwa kutokana na janga la kibinadamu mara nyingi upewa nafasi kumfikia
mlengwa kwa namna yoyote, iwe ni ulinzi au kutumia njia itakayoweza kuwafikia
walengwa.
MOJA KATI YA MAROLI YALIYOKUWA YAMEBEBA SHEHENA YA MSAADA< BAADA YA KULIPULIWA |
Hali ni tofauti pale
kunapotokea shambulizi juu ya chombo kilichobeba msaada, nchini Syria msafara
uliokuwa umebeba vyakula na vitu vingine kwa ajili ya watu waliokumbwa na vita
umeshambuliwa na ndege za kivita Jumatatu ya wiki hii katika mji wa Beirut.
Taarifa iliyotolewa na
Umoja wa mataifa inasema watu kadhaa wamekufa na wengine kujeruhiwa wakiwa na
hali mbaya. Vilevile msemaji mkuu wa umoja wa mataifa Stephen O’Brien amesema katika ripoti
inayoelezea kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine kuumia sana katika msafara huo akiwemo na Msiria
anayehudumu kwa kujitolea. (Volunteer)
Wakati mapigano nchini Syria yakichukua muda mrefu huku wananchi wakiendelea kutaabika, taarifa nyingine iliyosema, Rais Bashir Assad hayupo makini wala kujitoa kwa nia halisi, badala yake amekuwa akidhoofisha hali ya usalama, pamoja na kuwa angeweza kutoa msaada wa msafara huo kufika kule unapokwenda, ilisema taarifa hiyo.
Post a Comment