0

PICHA: Kamishina Generali wa Magereza nchini J.C Minja kulia aliyesimama akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini makao makuu ya Jeshi la magereza.











PICHA: Aliyesimama katikati; Mrakibu mwandamizi wa Jeshi la magereza nchini Lipina C.Lyimo, akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa sheria ya Bodi ya Parole nchini.








PICHA: Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini Dr. Augustino Lyatonga Mrema akisisitiza moja ya hatua ambazo Bodi yake imejipanga kuzichukua ili kuweza kupunguza msongamano wa wafungwa kwenye magereza nchini.





Baadhi ya watanzania wamekuwa wakijiuliza au kutaka kujua utendaji na maana halisi ya Parole inajihusisha na nini, lengo na makusudi yake hasa ni yapi?

Parole ni utaratibu unaowawezesha wafungwa wanaotumikia vifungo virefu magerezani kuaciliwa kwa mashariti maalum kabla ya vifungo vyao kumalizika, hivyo upelekwa hama kwenda kutumikia sehemu ya vifungo vilivyobaki katika jamii.

Mara nyingi wafungwa wanaofaidika na utaratibu huu hawasamehe wi vifungo vyao, ila hurudi katika jamii husika na kuendelea kutumikia vifungo vyao. Chini ya utaratibu huu jamii hupata fulsa ya kushiriki katika suala zima la kuwarekebisha wafungwa ikiwa ni pamoja na kuwajengea tabia njema na maisha ya kujitegemea.

Vile vile parole ina dhana yenye misingi inasaidia kutokuwepo wafungwa jeuri na wakorofi pia kudumisha nidhamu gerezani kwa kuwapa wafungwa sababu ya kuwa na mwenendo mzuri, dhana inayopelekea jamii kujihakikishia usalama zaidi hasa pale inapompa mhalifu nafasi ya kuendesha maisha halali yasiyo na makossa chini ya uangalizi na masharti  maalum kuliko anapotupwa gerezani kwa muda mrefu.

Hapa nchini magereza yanaruhusiwa kuhifadhi wafungwa 29552 lakini kutokana na wingi wa wafungwa 33,550 ikiwa ni sawa na ongezeko la wafungwa 3998 ikiwa ni nusu wafungwa na nusu ni mahabusi.

Hata hivyo mwenyekiti wa Parole nchini Mh.Augustine Lyatonga Mrema aliweka wazi nia ya bodi yake katika kushugulikia matatizo yaliyopo ikiwa ni pamoja na upungufu wa bajeti ambayo inaonekana ndiyo kikwazo kwa maafisa wa Parole kwenda kufuatilia na kutoa taarifa zinazowahusu wafungwa wanaotakiwa kupata nafuu hiyo.

Alisema "kama hakuna pesa, kama hakuna nauli tusitegemee miujiza hili ni tatizo kubwa, nitamwambia Rais kwamba ile kazi nakupongeza, nakushukuru, lakini sitaweza kuifanya kazi hii vizuri sa kwa sababu ya ufinyu wa bajeti na wabunge wajue, hauwezi kusema magereza imejaa wafungwa lakini haujui namna ya kuwatoa"

Aitha ili mfungwa aweze kupata nafuu hii ya Parole kuna sifa ambazo mfungwa anaweza kunufaika nazo; 
  1. Asiwe anatumikia kifungo cha maisha
  2. Asiwe ni mfungwa anayetumikia makosa ya unyang’anyi wa kutumia siraha, madaww ya kulevya na makossa yanayohusiana na kujamiiana.
  3. Asiwe amebadilishiwa adhabu au kupendekezwa kunufaika na mpango wa huduma kwa jamii kwa mujibu wa sheria ya huduma kwa jamii.
  4. Awe anatu,ikia kifungo kisichopungua miaka mine (4) au zaidi na awe ametumia 1/3 ya kifungo chake
  5. Awe ameonesha tabia na mwenendo mzuri kwa muda wote aliokaa gerezani.
  6. Asiwe na pingamizi la kimahakama la kukataliwa kunufaika na utaratibu wa Parole chini ya kifungu cha 67 cha sheria ya makossa ya Jinai.  
    PICHA YA PAMOJA: Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini Mh. Augustine Lyatonga Mrema mwenye suti nyeusi aliyekaa katikati akiwa na makamishina wa Jeshi la Magereza nchini wakiongozwa na Kamishina Generali Minja aliyekaa mkono wa kulia kwa Mwenyekit.

Post a Comment

 
Top