PICHA: Kijana/Mtoto Omran mwenye miaka minne (4) akiwa ameketi baada ya kuokolewa kutoka kwenye vifusi vya nyumba zilizolipuliwa Agosti 19. 2016.
Mtoto Omran mwenye umri wa miaka minne iliweka wazi jinsi madhila wanayopitia raia wa nchinini Syria hivi karibuni.
Mtoto huyo alionekana akiwa ametapakaa vumbi na damu mwilini baada ya kutekelezwa kwa shambulio la angani katika mji wa Aleppo nchini Syria.
Picha ya kijana huyo ambayo ilisambaa sana mtandaoni sawa na ilivyotokea kwa picha ya mwili wa kijana mwingine aitwaye Aylan Kurdi ambao ulipatikana katika ufukwe wa mjini Uturuki mwaka 2015.
Mara kadhaa watoto ukutwa sehemu ambazo ni nadra kufikilia kukuta mtu akiwa hai lakini pia mtoto huyu Omran mwenye miaka minne [4] aliokolewa kwa kutolewa kwenye vifusi baada ya kutekelezwa kwa shambulio la angani katika eneo la Qaterji, kusini mashariki mwa Aleppo nchini Syria.
Jamii ya kimataifa iliguswa hivyo wito wa kusitishwa kwa mapigano ulitolewa.
Hata hivyo mshirika mkuu wa Rais Bashar al-Assad, Urusi, imesema iko tayari kusitisha vita katika mji huo wa kaskazini kwa saa 48 baada ya shambulio hilo kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia waliokimbia mapigano na waliokosa makazi.
Watu wapatao 290,000 wameuawa na wengine wametoroka makwao katika vita vilivyoanza toka mwaka 2011 nchini Syria na zaidi wanakadiliwa kufariki huku wakiwa wameshikiliwa vizuizini kwa mujibu wa shirika la shirika linalotetea haki za kibinadamu la Amnesty International.
Post a Comment