0
Gari aliyokuwemo Mh. Suleimani Jafo mara baada ya ajali iliyohusisha na gari lingine.


Habari zilizotufikia ni kuwa naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo anusuria katika ajali iyohusisha magari mawili leo baada ya gari lake kupata ajali katika eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya Toyota Cresta iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari la waziri walikuwemo watu watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva wake na wote walitoka salama katika ajali hiyo.


Gari aina ya Toyota Cresta ambayo ilihusika katika ajali iliyotokea wilayani Rungwe.

Ameendelea kusema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo  walifanyiwa uchunguzi kuthibitusha endapo kama wameumia kwa ndani au la, Lakini kwa taarifa nzuri za daktari aliyewafanyia uchunguzi zilisema hawakuumia popote na hali zao ni njema wakiwa wazima.

Askari wa Usalama barabarani wakichunguza na kupima jinsi ajali ilivyotokea eneo husika.

Katibu tawala mkoa wa Mbeya aliendelea alitanabaisha kuwa; baada ya hapo Mh. Waziri aliweza kuendelea na safari kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge vilivyotarajiwa kuanza mapema leo.

Post a Comment

 
Top