Baadhi ya wakulima wa
mbogamboga jijini Dar es salaam bado wanaonekana kutumia maji yasiyo salama kwa
matumizi ya umwagiliaji wa bustani zao. Hali hii inatoka na baadhi ya maeneo
wanayolima bustani zao kuwa siyo rasmi kwa uzalishaji wa mazao hayo.
PICHA: Moja ya mfereji unatumika kumwagilia mboga hizo |
Waandishi wa TODAYS NEW
waliotembelea eneo la mwembe sigara wilayani Temeke wameshuhudia hali halisi,
pamoja na kutopata ushirikiano kutoka kwa wakulima hao lakini hali hiyo haikuwafanya
kushindwa kuona kila kinachoendelea.
Kwa kifupi upatikanaji
wa maji katika eneo hilo siyo wa uhakika ukizingatia ni eneo la viwanda hivyo
mtu anayefanya kilimo anapaswa kuwa na uhakika wa kupata maji yenye usalama kwa
afya za wale watakaonunua kwa ajili ya lishe majumbani, tofauti na
inavyoonekana eneo hilo kutumia maji yanayoonekana kutoka kwenye mifereji
inayoanzia Gongolamboto kuja eneo la uwanja wa ndege.
PICHA: Mwandishi akipita katikati ya bustani kuangalia uhalisia. |
Hata hivyo mmoja wa wakulima wa mboga katika
eneo hilo Mama Malyanzile alisema “Maji tunayotumia ni masafi ingawa yanaonekana
si salama kwa kuwa yanatoka kwenye mfereji”
Vilevile Mama huyo
ameongeza kwa kusema, “…sisi ni wakulima
na katika ulimaji wetu soko hatuna na kama hatuna soko na kama ni
wajasiliamali, soko letu lipo pale ilala Boma ambapo eneo ni dogo sana katika
kufanyia biashara kwa sababu wakulima wote wa mboga jijini Dar Es Salaam na
hata kutoka mikoa ya jirani uleta hapo kwa ajili ya masoko, kwa hiyo tunaiomba
serikali kutusaidia kuapata masoko ya biashara zetu”
Hata hivyo, ofisa habari wa shirika la reli la TAZARA alizungumza na mwandishi wetu juu ya wakulima wa mbogamboga kuingilia eneo hilo pasipo kibali cha kulima eneo hilo jambo linaweza kuleta msigano wa kutokuelewana pindi ukifika wakati ambapo matumizi ya eneo hilo utakuwa umefika.
Habari hii imeandaliwa na Roda Kimathi
Post a Comment