PICHA:
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza sala wakati wa ufunguzi wa kikao cha
Bunge leo Mjini Dodoma.
PICHA: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akijibu wakati wa kikao cha
bunge ambapo alisema serikali ipo katika uhakiki wa maombi ya maeneo mapya
utawala kwa kuangalia vigezo katika kuanzisha maeneo hayo.
PICHA: Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo
ya Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akijibu wakati wa kikao cha bunge ambapo
alisema serikali serikali itaendelea kuongeza udahili wa walimu wa sayansi
katika vyuo vya elimu ili kuweza kukidhi mahitaji husika.
PICHA: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (kushoto) akimueleza jambo
Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. George
Simbachawene.
NOTE: Wakati wa uchangiaji wa mjadara huo juu ya maafa hayo yaliyotokea mkoani kagera, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe alijibu swali wakati wa kikao hicho bungeni ambapo aliwaeleza wabunge kuwa
Katiba ya Nchi ibara ya 3(2) inaeleza kuwa mambo yote yanayohusu uandikishaji
na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiswa kwa mujibu wa masharti ya
katiba na sheria iliyotungwa ba Bunge.
PICHA: Waziri wa Wizara ya Mmabo ya Ndani ya Nchi Mhe.
Mwigulu Nchemba akijibu wakati wa kikao
cha bunge ambapo alisisitiza watanzania kufuata sheria za nchi na iwapo
utakiuka jeshi la polisi litachukuwa hatua bila kujali itikadi ya chama
chochote cha siasa.
PICHA: Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijini Mhe. John Heche
akichangia hoja kuhusu tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati wa kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma.
PICHA: Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Mhe. Prof. Anna
Tibaijuka akichangia hoja kuhusu tetemeko la ardhi mkoani Kagera wakati wa kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma
ambapo mbali na mambo mengine wabunge wamekubaliana kuchangia posho ya siku
moja kwa ajili ya wahanga wa tetemeko mkoani Kagera.
PICHA: Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akitoa taarifa ya serikali kuhusu tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni Mkoani Kagera.
PICHA: Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakisimama kwa dakika moja kuungana na wahanga wa tetemeko lililotokea
mkoani Kagera.
Post a Comment