0


Wito umetolewa nchi kwa vijana kujikita katika kilimo na miradi endelevu nchini itakayowawezesha kuwaepusha kuingia katika uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na ukataji miti ili kuchoma mkaa kwa lengo la kujipatia kipato, kupitia taasisi ya iitwayo RALEIGH International vijana watawezeshwa kuleta mwamko kwa jamii na serikali  ili waanze kusaidia makundi ya vijana wenzao yanayojihusisha  katika utunzaji mazingira  ambapo  shirika hilo huchukua vijana zaidi ya 500 kila mwaka kujitolea katika miradi ya shirika hilo.
Hayo yamesemwa na ofisa mawasilinao wa shirika hilo linalounganisha mataifa manne duniani kama vile Nepal, Nicaragua, Boneo na Tanzania Bwana Kennedy Mmari akiongea na vyombo vya habari mapema leo kwa kutumia kauli mbiu ya KUAZIMIA KUWA NA UCHUMI WA KIJANI, amesema mradi huo umejikita kwa wananchi kuweza kutoa mafunzo pia amemtaka kila mwananchi anapofanya shughuli za kilimo,ufugaji na nishati kuzingatia  kanuni za maendeleo endelevu na mazingira kwa kila kitu kinachofanyika.


Mmasi Ameongeza kuwa kutokana na watu wengi kutofuata kanuni za mazingira ambayo yamekuwa hatarini na kuwaathiri sana vijana kwa vizazi vijavyo, mfano ni katika mlima  Kilimanjaro theruji zimekuwa zikiyeyuka  na kutishia uhai wa viumbe kwa miaka ijayo.




Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava aliyekuwa mgeni rasmi  katika  kongaimano hilo lililogusa zaidi vijana kuhusu mazingira amesema;  Mifukoya plastiki imekuwa ni tatizo kubwa katika uhifadhi wa mazingira kutokana na kuendelea kuzagaa sehemu nyingi ikiwa ni nchi kavu au baharini imekwua ikisababisha hata injini za vyombo vya majini kama boti kuharibika na kuzima, hivyo ofisi ya makamu wa rais imejipanga kukabiliana na hali hiyo ambapo kufikia mwezi January mwakani (2017) mifuko hiyo haita ruhusiwa kuzalishwa na tayari imeshapigwa marufuku.

Katika hatua nyingine imethibitika kuwa Tanzania inapoteza zaidi ya hekta 372000  kila mwaka eneo linalokadiliwa kuwa sawa na ukubwa wa nchi ya Rwanda, kutokana na ukataji miti kwa matumizi ya nishati ya  kuni na mkaa, uchomaji wa misitu unaofanywa na baadhi ya Raia wasio waaminifu kwenye hifadhi mbalimbali nchini.

 PICHANaibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava mwenye suti aliyekaa katikati akiwa na viongozi wa RALEIGH pamoja na vijana washiriki wa kongamano.

Post a Comment

 
Top