0

Na Leonard Mutani. TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM
Wakati mbio za kuwania kiti cha kuliongoza Taifa kubwa kabisa duniani kwa uchumi na lenye propaganda za kila aina Marekani zikiwa zimebaki kwa wagombea wawili, Donald Trump kutoka Republican na Hilary Clinton kutoka Democratic, mbio hizo zinaonekana kuungwa mkono na wamarekani kwa kila mmoja kuamini mgombea wake atashinda.

Ikumbukwe hivi karibuni wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha luninga nchini marekani, Rais wa sasa anayeliongoza taifa hilo Barrack Obama, aliweka wazi msimamo wake kuwa Bwn Trump awezi kuja kuwa Rais wa marekani, na kwa kuonyesha kutokumuunga mkono alionyesha hisia kwa kutoa machozi, kitu ambacho kilionyesha ni kumdharau na kutokumuamini mgombea huyo wa Republican.

Kwa maoni ya wamarekani ambao ukiwauliza kuhusu Trump wanasema na kumuunga mkono kutokana na misimamo yake juu ya mambo ya ndani ya taifa hilo, hususani suala la ugaidi, japo amekuwa kama kinyonga kuhusu siasa za kimataifa, lakini kwa bibi Clinton ambaye miezi michache iliyopita alimzidi kwa pointi mbili triumph, hata hivyo kunaonyesha uwezekano na mashindano ya kuzua mgawanyiko mkali pamoja na mistari ya idadi ya watu katika siku ya uchaguzi.

Wakati bibi Clinton ikitokea kuwa Rais wa marekani  inasemekana ndiye atakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa mkubwa kama huo toka kuanzishwa kwa taifa hilo Julai 4, 1776, hata hivyo akiwa na matumaini ya kuungwa mkono wa Rais Barrack Obama anaweza kupata nafasi ya kupeperusha bendera ya USA?, ikiwa dhana ya 'ladies first' inakosa nguvu miongoni mwa wapiga kura wa jinsia ya kike kuonyesha kutokumuunga mkono!.

Hivi karibuni shirika moja la kimataifa lijulikanalo kama Economist Intelligence Unit (EIU) lilionya kuwa ushindi wa Donald Trump unachukuliwa kuwa ni miongoni mwa hatari 10 zaidi zitakazoikabili dunia endapo atashinda urais wa Marekani, na linasema huenda ushindi wake ukavuruga uchumi wa dunia na kuongeza hatari za kisiasa na kiusalama dhidi ya Marekani.

Hata hivyo, shirika hilo halimtarajii Bw Trump kumshinda Bi Hilary Clinton ambaye shirika hilo linasema *atakuwa na uwezekano mkubwa kushinda, kwa mtizamo wa kawaida unaweza kuangalia mvuto alionao Rais Obama kwa wamarekani na jinsi alivyoweka karata yake kwa bi. Clinton kuwania urais Marekani kwa tiketi ya Democratic, inaweza kuwa njia ya kumuangamiza moja kwa moja Trump ukizingatia Obama /wakati ule/ alipenya kwa vigezo kadhaa kimojawapo kikiwa ni cha kulifunga gereza la Guantanamo.

Ushindi wa Trump unaorodheshwa kuwa hatari zaidi kwa dunia kushinda hata Uingereza kuondoka kutoka kwa Umoja wa Ulaya au hata makabiliano ya kivita kule Syria au katika bahari ya South China Sea, kuyumba kwa uchumi wa china au Urusi kuingilia kivita Ukraine na Syria na kusababisha vita vipya vya chini kwa chini miongoni mwa mambo ambayo yanachukuliwa kuwa hatari zaidi ya ushindi wa wake.

Baadhi ya matamshi tata ya Bwn Trump ambayo aliyatoa akionyeshamsimamo mkali ni dhidi ya biashara huria, pamoja na kupendekeza ujengwe kati ya Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji lakini pia ametetea kuuawa kwa jamaa za magaidi, huku akipendekeza kuvamiwa kwa Syria ili kuangamiza kundi la Islamic State.

Post a Comment

 
Top