PICHA: Nchi za Africa Mashariki kabla ya Sudani kusini. |
Mkutano wa 17 wa wakuu wanchi za jumuiya ya Afrika mashariki uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam umemalizika kwa makubaliano ya jumuiya hiyo kuongezwa muda wa miezi mitatu ili mazungumzo zaidi yafanyike kabla ya kusaini mkataba wa kiuchumi na jumuiya ya ulaya EPA.
Akizungumza katika mkutano huo mara baada kikao cha siri cha wakuu hao mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais wa Tanzania Dr John P Magufuli amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya ugumu wa jambo lenyewe kwa kuwa linagusa maslahi ya uchumi moja kwa moja katika uchumi wa viwanda ukilinganisha na nchi za ulaya zenye viwanda vikubwa ambapo vitahatarisha viwanda vidogo vya Afrika mashariki.
Pia amesema, maslahi ya kodi karibu asilimia 45% ya mapato ya kodi nchini hutokana na kodi zinazotozwa kutoka nchi za ulaya hivyo kuruhusiwa kwa bidhaa kutoka ulaya kuingia bila kodi kutaikosesha mapato Tanzania hivyo kuendelea kwa mazungumzo kutasaidia kutafuta njia zaidi za kuona ni jinsi gani yatakavyo rekebishwa na kazi hiyo imeachwa mikoni kwa Secretariat ya jumuiya hiyo.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameipongeza Sudani ya kusini kwa kuwa mwanachama kamili wa jumuiya hiyo na ameiomba jumuiya ya Ulaya kutoiadhibu Kenya kwa kuiongezea ushuru/kodi katika bidhaa zinazouzawa katika nchi hizo.
Pamoja na hayo mwenyekiti amemwapisha Bwana Christophe Bazivamo kutoka Rwanda kushika nafasi ya naibu karibu Mkuu wa jumuiya hiyo.
Post a Comment