0
Leonard Mutani.
TODAYSPRO.BLOGSPOT.COM


Makampuni 100 yamepokea tuzo za "TOP 100 mid sized Companies" hapa nchini, utolewaji wa tuzo hizo unahakisi katika kukuza biashara na mfumo mzima wa makampuni yanayochipukia yaliyo katika ukubwa wa katikati.

Kutambulika kwa kampuni na kupewa tuzo, mara kadhaa utafiti unafanyika na kuweza kutambua juhudi zinazofanywa mpaka kufikia kuitambulisha chini kama Tanzania kuwa moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi katika makampuni yaliyo katika ukubwa wa kati, hivyo kuonyesha mafanikio na kuongeza utoaji wa huduma, kuonyesha biashara, ubora, na hata baadhi ya mafanikio hasa kwa wajasiliamali kutokana na historia yao ya nyuma.

Makampuni 100 yaliyohudhulia hafla ya utolewaji tuzo uliyofanyika jijini Dar Es Salaam katika ubumbi wa Mlimani city, wakati wa utolewaji wa tuzo hizo ulihudhuliwa na Dr. Adelhelm Meru Katibu Mkuu wizara ya viwanda, Biashara na Uwekezaji, aliyekuwa mgeni rasmi pamoja watendaji wa makampuni kadhaa nchini kama Jacqueline Woiso kutoka Bank M na wengineo, ulihitimishwa kwa kampuni ya FLIGHTLINK inayojihusisha na safari za angani kupewa tuzo ya ushindi.

Jameel Kassam ni meneja na muendeshaji wa kituo cha FLIGHTLINK Dar Es Salaam anasema kujituma, kushirikisha na kuwajibika ndiyo njia mojawapo iliyofanya wao kupata mafaniko hayo, akitoa shukurani kwa ofisi nzima ya Flightlink Dar Es Salaam ambao waliweza kuweka juhudi kwenye malengo waliyoweka na hatimaye kufika hapo.

Akiongea na TODAYS NEWS mara baada ya kupokea tuzo hiyo Jameel anasema "Anashukuru wandaaji wa tuzo hiyo kuona mchango wao kama kampuni iliyo kati kibiashara ya usafirishaji wa anga, lakini pia anaishukuru serikali kuendelea kuimarisha viwanja vya ndege vya mikoani kama Dodoma, Mbeya, Mwanza na kwingineko ambako wao Flightlink wana matarajio ya kutoa huduma muda wote katika sehemu hizo.

Kampuni hiyo pia inatoa huduma ya ndege ya wagonjwa (Air Ambulance) ambayo inaweza kumsafirisha mgonjwa mahali popote nchini na nje ya nchi kwenda kutibiwa.




PICHA: Jameel Kassam katikati wa kampuni ya FLIGHTLINK akipokea tuzo ya mshindi wa kwanza kati ya makampuni 100 ya ukubwa wa kati, kulia ni kwake ni Katibu mkuu wizara ya viwanda, Biashara na Uwekezaji, Kushoto ni Jaqueline Woiso Meneja mkuu wa Bank M.








PICHAJameel Kassam katikati akinyanyua juu tuzo baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza.






PICHA:  Washiriki katika ukumbi wa Mlimani City wakifuatilia ukabidhiwaji wa tuzo.
 

PICHAkampuni CSI ELECTRICAL LTD ya jijini Dar Es Salaam ilipokea tuzo ikiwa ni moja kati ya makampuni 100 ya kati yanayokuwa nchini. Anayekabidhi tuzo Ketah Shah katikati na kulia kwake ni Joanna ambaye ni Strategy and Compliance Manager mwenye gauni la zambalau na wamwisho kushoto ni QAQC Manager wa kampuni ya CSI ELECTRICLA LMT wakiwa na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.




Post a Comment

 
Top