PICHA: Mh Edward Lowassa. (Picha haina uhusiano na habari hii) |
Aliyewahi kuwa waziri
mkuu wa Tanzania akiwa mwanachama wa ccm na baadaye kujitoa kaika chama hicho
na kujiunga na chama cha upinzani Chadema Mh. Edward Lowassa ameelezea kile
kinachoendelea nchini huku akitoa maoni yake kwa kile kwa kinachofanyika kwa sasa.
Akizungumzia muelekeo
wa siasa za Tanzania Lowassa ambaye aliwahi kuwa mgombea Urais kwa kupitia tiketi ya chadema amesema kutokuwa na katiba mpya kunasababisha kutopata
kile wananchi wanachotaka kutokana na matokeo ya uchaguzi wa Rais kutohojiwa
na mahakama yoyote na popote, pia ameongeza kwa kusema “katiba mpya ndiyo solution
ya mambo haya”
Akizungumzia utendaji
wa Rais magufuri Lowassa anasema; “Kuna mambo
anafanya vizuri na kuna mambo afanyi vizuri, dhahili kuna vitu vilivyokuwa
vinawagusa watanzania kama utendaji hafifu na vitu vingine amevichukulia hatua
nadhani ni vizuri, lakini mimi naamini tunaweza kufanya vizuri uko mbele kuliko
yeye”
Akijibu swali alipokuwa akifanya mahojiano na
mtangazaji John Nene wa idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Nairobi juu ya ufisadi
Lowassa anasema “Kuna juhudi nzuri amefanya lakini
sisi tulipokuwa madarakani tulifanya vizuri zaidi.” Kwa upande wa nguvu
ambayo angeanza nayo endapo angepata ridhaa ya kuchaguliwa na kuingia ikulu
anasema angeanza na maslahi ya walimu hususani upande wa mishahara na posho ili waweze
kuwa na moyo wa kufanya kazi.
Post a Comment