0
PICHA: Las Luciano pamoja na tattoo yenye jina la Rais JPM
Moja ya kuenea kwa umashuhuri wa mtu ni kutokana na tabia au jambo fulani ambalo linagusa aina fulani ya watu kulingana na wakati ambapo muhusika anatenda au anafanya kitu tofauti na wengine na kitu hicho kinagusa hisia.

Takribani miezi si chini ya kumi toka Rais John Pombe Magufuri ashike hatamu katika nafasi kubwa kabisa ya kiutawala hapa nchini, kumekuwepo na baadhi ya wananchi na hata viongozi kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wakifuatilia kwa karibu kile ambacho anakifanya, ikionekana ni tofauti na viongozi mbalimbali wanaoshika hatamu ktk mataifa yao.

Jambo moja na ambalo limeleta changamoto ni jinsi hata baadhi ya watu kuvutiwa na utendaji wa Rais JPM, wengine wamepelekea kupata watoto na kuwapa jina la magufuri, pia kuna baadhi ya washabaki wa soka nchini Kenya wao wamekipatia kituo/tawi lao jina la magufuri kuonyesha kukubali kile anachokifanya au kuvutiwa na aina ya uongozi alionao.

Tukivuka mipaka zaidi katika bara la Africa, tunakutana na mwanamuziki mmoja anayeimba muziki nchini Jamaica ajulikanaye kwa jina la Las Luciano, huyu amevuka zaidi na kuamua kujichora jina la 'Magufuri' kwenye sehemu ya kifua chake, hali hii imetokana na utendaji yakinifu ambao mwanamuziki huyo anasema umejengwa kwa kusema; ni Rais mwenye maono, atishwi na jambo dogo lisilo na faida ya muda mrefu, uwajibikaji, urasimu, uzembe kazini, rushwa na matatizo yanayowakabili wananchi.

Kwa mtizamo kama huu, hali hii inadhihirisha kuwa kile kinachotendwa au kufanywa na serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania kinaungwa mkono wa raia mbalimbali duniani pamoja na kwamba wengine bado hawajatoa hisia zao juu ya Rais John Pombe Magufuri.

Aluta continue, endelea kufunga gidani za njuga zako JPM.

Post a Comment

 
Top