Meneja Biashara soko la hisa DSE, Mary Kinabo |
Meneja Biashara na
mauzo soko la hisa la Dar Es Salaam DSE Mary Kinabo amesema kuwa kupanda kwa
mauzo ya hisa katika soko hilo kumetokana na hali ya kiuchumi kutengemaa baada
ya wawekezaji wengi kujitokeza kununua hisa za kampuni ya bia nchini.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Bi Mary Kinabo amesema kuwa katika
wiki hii mauzo katika soko hilo yamepanda mara mbili ikilinganishwa na wiki
iliyopita ambapo mauzo ya hisa yalipanda kutoka shs 3.8bilioni hadi kufikia
9bilioni.
“Wakati huohuo idadi ya
hisa zilizouzwa na kununuliwa zimepanda kwa 49% asilimia, kutoka shs 724,000
hadi kufikia 1milioni” alisema Kinabo.
Pia alisema kuwa
kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni pamoja
na TBL kwa asilimia 54%, swiss port 16%
wakati CRDB ikishika nafasi ya tatu katika soko la hisa kwa kuwa na
asilimia 11% mapema hivi karibuni.
Bi Mary Kinabo
aliendelea kusema kuwa mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwenye 8.2trillion ikilinganishwa
na ukubwa wa mtaji wa soko uliopanda kutoka 20.8trillion hadi kufikia 21.3trillion.
“Sekta ya viwanda kwa
wiki hii imeshuka kwa 2.62 point baada ya bei ya hisa za TBL kushuka kwa 0.08%
wakati sekta ya huduma za kifedha imepanda kutoka 3.38% baada ya bei ya hisa
katika kaunta za DSE kupanda kwa 12.04%.” aliongeza Kinabo.
Vilevile aliongeza kuwa sekta ya huduma za kibiashara kwa wiki hii iko palepale baada ya
hisa za swiss port kubaki kwa bei ileile ya awali ya shs 3,543.02.
Post a Comment