FELIX MOSHA, IBRAHIM MADUMA na ANTHONY B. NYAKAJI |
Waanzailishi na wanahisa wa kwanza wa NICOL nchini Tanzania wakiongea
na waandishi wa habari juu ya malalamiko yao dhidi ya maamuzi ya mahakama kuu
iliyomrudisha mwenyekiti Mosha na Mtendaji mkuu wa NICOL Armstrong katika
nafasi zao na kukataza kuitishwa kwa mkutano mkuu wa wanahisa.
Pia walikanusha madai kwamba NICOL imeshindwa kuendelea na
ilishakufa kuweza kutoa huduma, hata hivyo katika kuelezea mafanikio
waliyofikia Ferix Mosha ambaye ni Mwenyekiti wa NICOL amesema waliweza kufanya
mazungumzo/mawasiliano na Dangote ilia aje nchini kufanya uwekezaji na ambapo
kupitia wao ndipo uwekezaji mkubwa ulifanyika mkoani Mtwara kwa kujengwa
kiwanda kikubwa cha cement umefanikiwa.
Post a Comment