PHOTO:
Kulia, Kamana Stanley -Mkurugenzi msaidizi utekelezaji Katiba.
Kushoto, Sheiba Bulu -Afisa
Mawasiliano serikalini.
____________________________
Wakati sheria haikuwa wazi kuwalinda wananchi na wale
waliokuwa wanatoa taarifa za matendo, matukio yoyote ya kiuhalifu, mwaka 2015
serikali iliwasilisha Bungeni muswada wa sheria kuwalinda mashahifi na watoa
taarifa, hii ni katika kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu
nchini.
Dkt Harrison Makyembe amabye ni waziri wa mwenye dhamana ya
usimamizi wa sheria nchini, aliidhinisha na baadaye kupitishwa kuwa sheria ya
kuwalinda watoa taarifa za uhalifu na mashahidi tarehe 25 Marchi 2016, ambapo
sheria hiyo ilitangazwa katika gazeti la serikali.
Katika sheria hiyo, wale wote wanaofanikisha kuokoa mali ya
umma, kupatikana kwa wahalifu,kulinda mazingira na maisha ya binadam kutokana
na uhalifu uliopangwa kufanyika lakini uhalifu huo kuzuiliwa kutokana na
taarifa iliyotolewa katika mamlaka husika.
Vilevile uwepo wa sheria hii kutasaidia kuwapatia ulinzi wa
kisheria wote wanaotoa taarifa za uhalifu na makosa mbalimbali wanayokusudia
yakitendeka na itarahisisha utoaji na upatikanaji wa taarifa, kwani taarifa za
uharifu kwa sasa zitatolewa pia kupokelewa si katika vyombo vya dola pekee bali
hata kupitia vyombo vya habari na vyanzo vingine vinavyoainishwa katika sheria
husika.
Lakini wote watakaoshindwa kushugulikiwa vyema taarifa
zinazotolewa kwao na kuruhusu watoa taarifa na mashaidi kupata madhara, basi
sheria imeweka utaratibu wa namna ya kushughulika nao. Wananchi wanaimizwa
kujitokeza bila uoga kutoa taarifa za uharifu dhidi ya matendo ya aina yote
yanayofanywa kinyume cha sheria, hivyo kuisaida serikali katika mapambano dhidi
ya uharifu na kujenga jamii na taifa linalopinga uharifu.
Aitha inatarajiwa uwepo wa sheria hii kutaleta matokea chanya
katika mapambano na uharifu wa aina zote na yataimarika kutokana na kuwepo kwa
utayari wa wananchi kushiriki kufichua maovu ikiwa ni pamoja na yale
yanayosababisha hasara kwa taifa kwa ujumla.
Post a Comment