Kitabu/Kamusi chenye ujumbe wenye kuweza kumsaidia mkristo na mtu yeyote anayependa kukuza taaluma kupitia maneno ambayo yanaweza kumjenga msomaji wake.
Bi Lilly Beleko ambaye ni Kaimu mkurugenzi wa Utamaduni, akisoma hotuba kwa niaba ya waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo katika ofisi za balaza la maaskofu kurasini jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya masista na wafanyakazi wa balaza la maaskofu Tanzania wakimsikiliza kwa makini mwakilishi wa Waziri Bi Lilly Beleko, hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa kitabu/kamusi.
Mzee kuboya ambaye ni kati ya watu waliofanikisha uchapaji wa kitabu/KAMUSI YA UKRISTO, akitoa uhalisia wa jinsi uandaaji wake ulivyofanyika huku akitoa angalizo juu kwa watanzania kupendo kusoma vitabu.
PadriUbaldus Kidavuri ambaye ni mkuu wa idara ya walei ya Balaza la maaskofu katoliki Tanzania
(TEC) akitoa neno fupi katika hafla ya uzinduzi wa KAMUSI YA UKRISTO
Lakini pia alishukuru kuona tukio hili likitokea kwa mara ya kwanza katika historia ya kanisa katoliki nchini Tanzania.
Pia kwa jinsi serikali inavyothamini jitihada za ukuzaji wa elimu na hasa Imani
.
Ndugu Seleman Sewangi katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Tanzania akielezea jinsi Kamusi hiyo ilivyo oanisha maneno ambayo wengi wa watumiaji wake hasa wakristo wanavyokosea kuyatumia katika matumizi halisi.
Baadhi ya wageni waliodhulia hafla hiyo wakiendelea kusikiliza kila hatua kile kinachoelezwa na na wataalam waandaaji waliohusika katika kufanikisha kuchapishwa kamusi hiyo.
Padri, Daktari JORDAN NYENYEMBE ambaye ndiye mwandishi na mtunzi wa kitabu KAMUSI YA UKRISTO akitoa maneno machache na kumshukuru Mungu kuweza kufanikisha kuchapwa kwa kamusi hiyo ambayo itapatikana Nchini kote katika maduka ya vitabu.
UKATAJI UTEPE: Ukiongozwa na Bi Lilly Buleko -mwakilishi wa waziri (katika) kushoto kwake Padri Dr. Jordan Nyenyembe na kulia ni Padri Ubaldus Kidavuri wakishiriki zoezi hilo.
KAMUSI YA UKRISTO: Ambayo imezinduliwa kwa niaba ya waziri wa Habari, Utamadunu, Sanaa na Michezo Nape Nnauye na Bi Lilly Bulek
Post a Comment