Mkurugenzi wa Habari maelezo nchi ndg Hassan Abas akiongea na waandishi (hawapo pichani) wa Habari juu ya mpango wa serikali juu mawaziri wote walio katika balaza la mawaziri kuonekana zaidi kwenye vyombo vya habari.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, wakihusika katika uchukuaji wa taarifa iliyokuwa inatolewa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari Maelezo akiyekaa akiandika, akiwa makini kujibu swali la mwandishi wa habari lililohoji juu ya vyombo vya habari hasa vya magazeti kunyimwa nafasi kwenye dhifa mbalimbali za kitaifa.
HABARI KAMILI:
Katika hali ya kuongeza utendaji na uwazi kwa
serikali iliyopo madarakani, serikali imeamua kuja na njia ya kushirikiana na
vyombo vya habari ikiwahusisha mawaziri katika hatua hii mpya, ambayo
inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa hapa nchini.
Kuanzishwa kwa hatua hii kutaleta nafasi kwa
mawaziri na ofisi zao kuweka wazi vipaumbele vyao vya bajeti ili wananchi
waweze kujua ikiwa ni pamoja na changamoto na mafanikio yatakayofikiwa kwa
wakati.
Mkurugenzi wa habari maelezo, ndugu Hassan Abas
akiongea na waandishi wa habari juu ya hatua ambayo serikali imefikia kwa mawaziri
wote kuwa na uhusiano/ushirikiano na vyombo vya habari. Katika hatua nyingine wiki
ijayo, anatarajiwa kuanza ziara ya kushitukiza kwenye vyombo vya habari hapa
nchini ili kuangalia hali halisi ya utendaji na ushilikishwaji wa waandishi wa
habari katika vyombo hivyo.
Hali kadhalika, njia hii haitakuwa ya mara moja kwa mawaziri
hao bali itakuwa endelevu ili kila mwisho wa mwezi watapaswa kutoa report zao
juu ya utendaji wa wizara zao. wanatakiwa
Katika hatua nyingine idara yake imeanza mchakato
kwa waandishi wa habari kupata nafasi ya kuongeza ujuzi nje na ndani ya nchi,
ambapo amsemea atalifanyia kazi na kulipa kipaumbele ili kupata nafasi ya
kubadilishana uzoefu na wanahabari wengine.
Aitha pamoja na kutoa historia yake fupi toka
alipokuwa mwandishi wa kujitegemea mpaka kufikia hatua aliyopo sasa, bado
anaona vyombo vya habari haviwapi nafasi yoyote waandishi hao pale wanapopeleka
habari na analitambua hilo huku akiahidi kulifanyia kazi kuweka uhuwiano sawa,
alitolea mfano mashirika makubwa ya habari duniani kama DW, BBC n ahata CNN
kuwa yanapokea habari kutoka duniani kote kutoka kwa waandishi wa kujitegemea.
Post a Comment