0




Ndugu Joseph Mabusi kulia akikabidhi moja ya madawati kwa mkuu wa wilaya ya Ilala aliyeshikana naye mkono, aliye pembeni mwa mkuu wa wilaya ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Jitihada, Zainab Sambari.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema Akiongea na waandishi juu ya madawati yaliyotolewa na Diamond Trust Bank.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Jitihada akitoa shukurani kwa wadau waliotoa madawati makabidhiano yaliyofanyika ofisini kwa mkuu wa wilaya ya ilala.
Mkuu wa idara ya fedha kutoka Diamond Trust Bank mwenye suti akimuonyesha na kumueleza mkuu wa wilaya ubora na umadhubutu wa madawati waliyoyakabidhi.
Mwenyekiti wa shule hiyo ndg.Isack Kibiti akitoa hamasa, maoni kwa wanafunzi na walimu kutunza mali zinazotolewa na wadau wa elimu ili zidumu.
PICHA: Ikijumuisha wadau wafanyakazi wa Diamond Trust Bank, Walimu kutoka Jitihada shule ya msingi, Mwenyekiti wa shule na mkuu wa wilaya ya Ilala mwenye kiremba.


Kufuatia agizo la Mh. Rais John Pombe Magufuri la kuhakikisha halmashauri zote nchini, zinahakikisha shule za msingi na sekondari zinajitosheleza kwa madawatikwa  mwaka huu 2016, hivyo wadau mbalimbali wamekuwa wakimuunga mkono Rais ili kuweza kufikia lengo hilo.

Akikabidhi madawati hayo, mkuu wa idara ya fedha wa Bank hiyo ndg. Joseph Mabusi anasema, “Pamoja na kumaliza vyumba viwili vya madarasa , bado vyumba hivyo havikuwa na maana endapo vilikuwa havina madawati” kufuatia kauli hiyo, DTB waliona haja ya kutengeneza madawati 50 kwa ajili ya madarasa hayo.

Hata hivyo, shule hiyo ilikuwa haina viti na meza kwa ajili ya walimu ambapo DTB waliahidi kutengeneza meza na viti kwa ajili ya walimu ambao hapo awali walikuwa wakitumia madawati ya wanafunzi kama meza zao.

Hali kadhalika Bank hiyo imeendeleza juhudi za serikali za kila mwanafunzi akae kwenye dawati na kutengeneza madawati yapatayo 200 ili watoto waweze kusoma katika mazingira rafiki pamoja na walimu kufundisha vyema.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema amepokea madawati yaliyotolewa na Bank ya Diamond Trust Bank ikiwa ni muendelezo wa Bank hiyo katika kutimiza ahadi waliyoitoa wakati wakikabidhi majengo wa madarasa kwa shule ya msingi Jitihada iliyopo kata ya kitunda wilaya ya Ilala.

Pamoja na shukurani kwa Bank hiyo DC Sophia Mjema, aliomba wadau wengine wa maendeleo au mwananchi yeyote anayeguswa anapaswa kutoa kitu chochote kinachoweza kugusa secta ya elimu hata cement, nondo, mabati nk, ili kuendeleza juhudi za mh. Rais kwa kutoa elimu bure kutoka darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.

Mwalimu mkuu  wa shule hiyo Bi. Zainab Sambari pamoja na Mwenyekiti wa Shule hiyo Bw. Isack Kibiti wanawaomba walimu kujituma kufikia malengo, kutokana na juhudi zitokanazo na wadau kuchangia elimu. ‘Kila mtu akitimiza wajibu wake na rasilimali zikatumika inavyotakiwa, bila shaka kila mtoto anaweza kukaa kwenye dawati, pia kuwepo kwa vyumba vya madarasa vya kutosha.

Post a Comment

 
Top