0

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO Mh. Nape Moses Nnauye (mB)

Wakati kukiwa na harakati kwa vyombo vya habari kuwa huru kutoa habari huku habari hizo zikichujwa na kumfiki mwananchi zikiwa hazina ishara yoyote ya uvunjifu, kuashiria kuegemea upande ambao unakinzana na maadali ya uandishi wa habari.

 Kutokana na vifungu vya sheria na kanuni  ya 5 (a), (b), (c) na (d ) ambavyo vinavyozuia kituo chochote cha Redio nchini kutoa lugha yenye maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa Amani na hivyo kukiuka masharti hayo na kanuni ya 6(a), (b), (c) na 18 (i), (ii) na (iii) ya kanuni za utangazaji za mwaka 2005.




Kwa mamlaka aliyonayo waziri chini ya kifungu cha 28(1) cha sheria ya mamlaka ya mawaliano Tanzania yam waka 2003, amevifungia kwa muda vtuo vya Redio Five cha Arusha na Magic FM cha Dar Es Salaam. Wakati huohuo ameielekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo ili kuwasikiliza kwa kina zaidi na kumshauri waziri kwa hatua zaidi

Waziri Nape amevitaadharisha  vyombo mbali mbali vya habari kutoshawishika kuvunja sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari, ili kulinda heshima ya tasnia na wakati huo kuhakikisha nchi yetu inabaki na Amani, Ushirikiano na Umoja.

Post a Comment

 
Top