Katibu wa Chama cha Tanzania Drama Film Actors Assosiation ndugu Jaffar Makatu mwenye kibaraghashee akiongea kuhusu mipango ya chama mapema leo.
Chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni Tanzania Drama Film
Actors Association TDFAA Kimeitaka serikali kupitia wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na michezo kuharakisha sera ya filamu ambayo itaoanisha mambo mbalimbali ya
kisheria katika tasnia ya filam.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katibu wa chama Jafari Makatu amesema kuwa, ili
filamu na tasnia za nchini zibebe ujumbe ulio bora ni lazima kuwe na sheria za
uandaaji wa kazi, masoko, haki miliki na malipo stahiki kwa kila kazi, pamoja
na ulazima kwa kila msanii na mtendaji kujiunga na katika vyama husika na kufanya
kazi zenye ubora.
Pia amemuomba Mh. Rais John Pombe Magufuri kuwatengea ardhi ya kuigizia kwa kutengeneza mahakama,vituo vya
polisi nk,pia wasanii kuwa na unifomu itakayoweza kuwatambulisha kama vazi
maalumu la kipolisi kwa wasanii wa Tanzania ama mwigizaji yoyote atakae kuja
kuigiza katika ardhi ya Tanzania.
Habari imeandaliwa na Roda Kimath.
Post a Comment