Ili uweze kukidhi kutunza na kufuatilia misitu,
fedha ni moja la hitaji muhimu sana katika nyanja hii, kutokana na mazingira ya sector hii yalivyokaa, lakini pia uharibifu wa misitu ni mkubwa kuliko uhalisia unavyotajwa
katika makabrasha, mojawapo ni jinsi watu wanavyovuna miti kwa wingi huku wakikata mbao bila vibali na kuchoma kuni, ikiwa wizara
imetulia huku vitendea kazi vya wasimamizi vikiharibika pasipo kufanyiwa matengenezo, mfano boti za doria zilizo mikoa ya kusini.
Mmoja wa watoa mada kuhusiana na misitu nchini Mzee Kahana Lukumbisi
akitoa maoni na mapendekezo kwa wadau wa misitu na serikali.
Hali hii inapelekea kuwapa upenyo wavunaji haramu kuvuna na
kusafirisha bila wasiwasi, hata hivyo baadhi ya wilaya kusini mwa Tanzania fedha
nyingi zinatokana na misitu lakini bajeti ya kushugulikia suala la misitu
haikidhi haja, na inapelekea maafisa misitu kutoweza kufikia malengo.
Ripoti ya misitu inaonesha kuwa wizara ya maliasili haitoi
ushirikiano kwa ngazi za chini ipasavyo.
Serikali iweke kipaumbele kwa kununua vitendea kazi kwa
ajili kulinda misitu na kusimamia misitu ya asili, vilevile miongozo
itakayopelekwa ngazi za chini ili kuwepo na wigo mpana wa kulinda misitu. Wakati
ushuru wa aslilima 5% ya misitu hurudi serikali ya mtaa, serikali inapaswa
kuliangalia upya ilo ili kuweza kuwapa bajeti zaidi.
Mwakilishi wa balozi wa Finland nchini Bw.Simo pekka Parviainen.
Wakati kukiwa na mabadiriko makubwa kuhusiana na sector ya misitu,
serikali ya Finland imekuwa mstari wa mbele kutoa msaada sehemu mbalimbali
ikiwepo kwenye kampeni ya Mama Misitu ili kuweza kutoa changamoto kwa wananchi kutunza
misitu, serikali ya Finland ilitoa kiasi cha euro 10milion mwaka 2006 katika kuendeleza juhudi
za uhifadhi wa mazingira nchini Tanzania.
Hata hivyo bado kuna msisitizo mkubwa unahitajika kwa serikali kuwapa elimu wananchi wa vijijini ambao wanaonekana ndiyo wakataji wakubwa wa mazao ya misitu kuepuka na uharibufu huo.
Waziri na Maliasili na Utalii nchini mh. Jumanne Mghembe
Cha kwanza
kinachofanya tuweze kuishi hapa duniani ni misitu, hivyo tunapaswa kuitunza
sana kuliko kitu kingine, na ikitizamwa duniani kote Tanzania tulipaswa kuwa na
joto sana lakini kwa sababu serikali imeweka asilimia kubwa ya mraba wa eneo la
misitu, hali hii inatufanya tuweze kuwa na hali ya hewa nzuri.
Pamoja na yote hali ya uvunaji miti nchini imekuwa siyo
nzuri ikiwa na maana vyama vya wavunaji ni vingi kuliko vyama vya wapandaji
miti, hali hiyo inaonesha umuhimu wa kuweka sheria zitakazosaidia kuwepo kwa
vyama vya wapandaji ambavyo vitapewa nafasi ya kwanza kuvuna misitu.
Tatizo linaloonekana kwa sasa na ambalo tunalifanyia kazi; hakuna
utaratibu wa kusafirisha mazao ya misitu ambapo msafirishaji yeyote
anayesafirisha mazao ya misitu usiku, mali zote kama gari na mbao vitataifishwa akiwemo na muhusika kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.
Hata hivyo waziri magembe amesema katika kuongeza hamasa kwa wapandaji miti nchini, serikali
imeanzisha mfuko maalum wa kuwasaidia wananchi wote watakaojihusisha na
upandaji miti.
Post a Comment