Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi Leticia
Ghati Mosore ambaye kwa sasa amevuliwa uwenyekiti na uanachama, amesema kuwa
hatambui kusimamishwa uanachama na uwongozi kwa sababu hajapewa sababu za
kusimamishwa kwake wala barua yenye kuelekeza vifungu vya katiba na kanuni
zilizo tumika kufikia maamuzi hayo.
Amesema hayo mapema leo alipozungumza na waandishi wa habari
huku akisema kuwa mgogoro wao unafahamika na Mwenyekiti James Mbatia ila
anajaribu kuficha ukweli kwa kuzusha maneno mengi na tuhuma nyingi za uwongo
kuukwepa ukweli.
Hata hivyo amesema kuwa hakutaka kuanzia mahakamani kwa sababu
hata walivyo mtangaza kumvua uongozi na uwanachama walianzia kwenye vyombo vya
habari, pia hatoweza kwenda chama kingine ila ataanzisha chama chake cha
wanawake.
Alimalizia kwa kusema NCCR imeporomoka kwa kiasi kikubwa
kutokana na mwenyekiti wa chama James Mbati kutoonyesha ushirikiano na
wanachama wenzake na kuwaacha wakiwa wananyanyasika ndani ya UKAWA.
Post a Comment