0
Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa kulia aliyejishika bega akimsikiliza Mbunge wa singida mashariki kushoto Mh. Lissu nje ya makao makuu ya jeshi la polisi kabla ya kuitwa ndani.


TAARIFA ZILIZOPO:
Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo wameitwa makao makuu ya kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano, hilo limejiri baada ya chama hicho kuendelea na mkutano wao wa ndani uliokuwa ukiendelea katika hotel ya Giraffe Hotel jijini Dar Es Salaam.

Wakati wajumbe kadhaa wakiwa ndani ya kituo kikuu kwa mahojiano wakiwemo Aliyekuwa mgombea kiti cha urais kupitia Chadema na aliyewahi kuwa waziri mkuu Edward Lowasa, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, Katibu mkuu Vincent Mashinje, Naibu katibu mkuu bara John Mnyika na baadaye mh. Lisu mbunge wa singida mashariki naye aliekea polisi.

NEWS UPDATES:
Viongozi waandamizi waliokuwa wakihojiwa kwa kukiuka sheria za kufanya mikutano ya ndani pasipo kibali cha jeshi la polisi waachiwa kwa dhamana.

Mwenyekiti wa Chadema katikati, Mbunge wa kawe Halima Mdee kulia na wakitoka kituo kikuu cha polisi majira ya 01:20 usiku baada ya kupata dhamana.


VIDEO: Alichokiongea Mh. Mbowe mara baada ya kupata dhamana, pamoja na kuwa walikuwa na kikao cha kamati kuu ya chama, ambacho kilishirikisha wabunge, mameya na wenyeviti wa halmashauri zinazoongozwa na Chadema nchi nzima, alikuwa na haya hapa...

Post a Comment

 
Top