0
AKWILIMA KAYUMBA: Mkurugenzi wakala wa usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA) nchini
Akiongea jambo wakati wa mkutano wake kwenye ukumbi wa habari maelezo kuhusiana na Upimaji wa Afya kwa waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema OSHA itaendesha zoezi maalum la upimaji afya za waliokuwa wafanyakazi wa uliokuwa mgodi huo ambao waliachishwa kazi na mgodi huo mwaka 2007.
Akiongea na waandishi wa habari alisema; Kulikuwa na ukiukwaji wa sheria kulipotiwa kwa wakala, na hatua zilichukuliwa ikiwemo kufanya ukaguzi maalum wa kiafya katika eneo la mgodi na kutoa onyo kali kwa mwajiri wa walalamikaji.

Pamoja chama wa wafanyakazi hao TAMICO pia kushiriki vikao vya usuruhishi, vilivyoshirikisha serikali, mwajili (Mgodi wa Bulyanhuru) pamoja na wafanyakazi hao.
Mpaka kufikia sasa waathirika 315 kati ya 371 ambao mwajili alithibitisha walikuwa wafanyakazi wake, wameshapimwa afya zao na waathirika waliobaki 56 hawakujitokeza wakati wa zoezi hilo.

Kwa waathirika ambao madaktari watagundua matatizo yao ya kiafya yamepatikana wakiwa kazini kutokana na kazi walizokuwa wanafanya, OSHA inashauli kufidiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Aitha waathirika ambao hawatakuwa na matatizo yoyote ya kiafya watapatiwa vyeti (Certificate of fitness) ambavyo utolewa kwa wafanyakazi waliofika ukomo wa ajira ao kwa mujibu wa kifungu Na.24 (2) cha sheria ya usalama na Afya mahali pa kazi ya mwaka 2003.

Upimaji ni mwendelezo wa hatua mbali mbali zinachochukuliwa na serikali katika sehemu mbalimbali za kazi, na inapaswa mwajili yoyote kuchukua hatua stahiki kuepusha migongano toka kwa wafanyakazi wake wakati wote kabla ya kustaafu au kufika ukomo wa ajira kwa mwajiliwa.

Mkurugenzi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi, Bi Akwilima Kayumba (katikati), Mkurugenzi wa Afya ndg Alex Ngata (kushoto) na Meneja Afya ndg Gershon Rweyange.

Post a Comment

 
Top