0



Wakati mwezi wa tisa/September mosi huwa hakuna tukio lolote kama sikukuu inayopelekea watanzania walio wengi kujipanga kwa maandalizi ya aina yoyote ihusuyo matumizi ya fedha au watu kupika vyakula ikihashilia sherehe ya aina yoyote au hata kwa mavazi.
 
Kupatwa kwa jua ni nini?

Kwenye mfumo wa mzunguko wa dunia, jua na mwezi kuna uwiano tofuti unaopelekea kila kimoja kufuata njia yake, wakati mwezi unapokuwa kwenye muelekeo wake ufikia wakati unakutana na jua kwenye usawa wake unaoelekeana na kufikia hatua ya kulifunika jua kwa takribani masaa manne (4) hapo ndipo tukio hilo la aina yake utokea.

Mara ya mwisho tukio hili lilitokea mji wa Christchurch, nchini New Zealand, ambapo lilishuhudiwa na wakaazi wengi waishio nchi za jirani ambapo wapo eneo ndani ya mita 100, hivyo hali hiyo ufanya baadhi ya raia kutoka nchi nyingine kusafiri umbali mrefu kufuata tukio hili la kipekee sana.
Kwa mara ya kwanza katika ukanda wa nchi za Africa mashariki tukio hili kubwa la aina yake la KUPATWA KWA JUA linaenda kutokea nchini Tanzania hususani ukanda wa nyanda za juu kusini mkoani Mbeya wilaya ya Rungwe eneo ambako tukio hili litaonekana kwa uzuri sana, lakini kuna sehemu za ukanda ambazo ukanda unakatisha ndani ya mita 100 kama vile Congo Songea, Masasi, Ruvuma mpaka Msumbiji, katika sehemu hizi wanaweza kuliona jua liliwa jembamba sana kama mfano wa pete.

Na inawezekana kuwa kama tukio la kawaida sana masikioni mwa wananchi ila kwa mtizamo tofauti ni tukio kubwa ambalo katika uhai wa mwanadamu mara nyingi hutokea ndani ya miaka 15 au zaidi kufikia tukio jingine na inategemeana na wapi utokea. Kwa vile asilimia 98 ya jua litakuwa limejificha nyuma ya mwezi  kunaweza kuonekana vema kwa watazamaji lakini kwa kutumia vifaa maalum vya kujikinga na miyonzi

Tukio la KUPATWA KWA JUA ni la kusisimua sana pia ni nadra sana kutokea kwenye maisha ya binadamu, ukizingatia kwenye hiki kizazi kipya ambacho kimechangamka sana hivyo kitasisimuliwa kutokana na tukio hili na watajifunza sayansi pasipo kuwa darasani; kwa nini kunatokea tukio hili.
Lakini hapa naangazia sehemu ambapo tukio hili linaenda kutukia, September 01.2016 ni siku inayoangukia alhamisi wanafunzi na wasomi mbalimbali watakuwa masomoni, hivyo linaweza kutumiwa na shule, taasisi za elimu kuendeleza sayansi na kuvuta wanafunzi kujiendeleza hasa upande wa sayansi inavyofanya kazi, hali hii itaongeza uelewa na ni muhimu katika kuelewa maumbile ya ulimwengu wetu.

Muda unaotegemewa kutokea kwa tukio hili ni kati ya saa 4 asubuhi mpaka 8 mchana hapo katikati kuna masaa manne (4) ya kufuatilia tukio hili, kwa wataalu, wanafunzi, wanavyuo na wote wanaojihusisha na mambo ya anga ni nafasi ya kufanya utafiti, kushirikiana na kuandika ripoti kwa kumbukumbu za baadaye.

Kuangalia tukio kwa uzuri zaidi haitakuwa kwa kutumia macho ya kawaida, ila kuna vifaa maalum vya kukingia macho ambavyo vinachuja mwanga  wa ju, mara nyingi vinafahamika kama kitazama jua.
Kutokana na maoni ya wataalam: Ni hatari sana kuangalia jua kwa macho ya moja kwa moja au kutumia vichujio vingine vya kiza vilivyotengenezwa kienyeji. Kifaa maalum kimoja kwa kawaida kinauzwa bei isiyozidi 500/-

Tunashauri wakaazi wa eneo ambalo tukio hili ka kipekee linaenda kutukio wawe wakalimu kwa wageni wengi wanajiandaa kuja katika siku za hivi sasa, lakini pia kuchukua fulsa ya kupata fedha kutoka kwa wageni kutokana na bidhaa nzuri na hata chakula na vinywaji.

HABARI HII NI:
Imeandaliwa na mwandishi Leonard Mutani pia kwa msaada mkubwa wa Dr, Noorali T. Jiwaji wa chuo kikuu Huria cha Tanzani.




 Mara kadhaa hali hii ya kupatwa kwa jua uonekana hivi, upande mmoja kuwa na kiza na mwingine miyale ya kuonekana.

Baadhi ya maeneo hali kama hii itatokewa kwa wataalam, watalii na hata watafiti kujiandaa eneo husika kwa ajili ya kupata picha malidhawa.


         Hii ni mojawapo ya miwani ambazo utumika wakati wa tukio la KUPATWA KWA JUA.

Wanafunzi na Wanavyuo wapewe nafasi kujifunza kuhusu sayansi hii ya Kupatwa Kwa Jua, iwe msaada kwao kwa ajili ya wale ambao hawatakuja kuona kwa siku za usoni.


 Huko ughaibuni kwa wazungu wao huwa wanalichukulia tukio hili kama la kihistoria na ufikia hatua wanakusanyika kwenye viwanja vikubwa kama vya mpira au pale panapoandaliwa na serikali kwa ajili ya kuweka kumbukumbu muhimu ya tikuo hilo.

Post a Comment

 
Top