Moja ya ajenda ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh. John Pombe Magufuri ni katika maendeleo ikiwemo upande wa elimu. wakati hilo likijili, baadhi ya shule nchini zimefanya uchaguzi kuwapata viongozi wa kamati za shule ambao watawakilisha na kusimamia maendeleo, mapato na utolewaji wa elimu bora kwa watoto walio katika shule husika.
Wazazi wakifuatilia maelezo kutoka kwa ndugu; David Maleko (hayupo pichani) kuhusu umuhimu wa kamati ya shule, na nini wanapaswa kufanya kuelekea kuwapata wanakamati hao.
Mara baada ya maelezo ya kina wazazi walipiga kura kuchagua kamati ya wazazi {5} na walimu {2} watakaowakilisha wazazi wote wenye watoto wanosoma shule ya msingi ununio pamoja na walimu hao wawili wa taaluma.
Aliyekaa wa kwanza ni Mwl mkuu wa shule hiyo ndg G.A Shayo akisoma malengo watakayoyafanyia kazi na kamati mpya. Baada ya kupiga kura, zinahesabiwa na kujua nani na nani wanoingia kwenye kamati ya utendaji.
Jumla ya kura zilizopigwa ni 292 kutokana na mgawanyo wa namba zilizopangwa kutoka 1-10, kati ya hizo namba 2 na 8 walijitoa.
Wazazi wakifuatilia uhesabiwaji wa kura walizopiga kuwapata wawakilishi wao kwenye kamati ya shule ya msingi ununio, wilaya ya kinondoni.
Ndugu David Maleko aliyenyanyua mkono ishrara ya kuongea, alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi alimwakilisha mratibu wa elimu kata ya Kunduchi jijini Dar Es Salaam.
WASHINDI: Kamati mpya ya shule iliyopatikana majina yao na kura kwenye mabano, kutoka kushoto; Mohammed Juma [31], Vicent Kutika [66], Fatuma Mwenda [45], Issa Suleiman [41] na Stephano Ndono [35]
Picha; Leonard Mutani



Post a Comment