Bunge la
seneti nchini kenya limepitisha sheria kwa kampuni mashirika mbalimbali nchini humo
kuweka sehemu maalum kwa ajili ya kuwanyonyeshea watoto wachanga.
Mbunge machachari mama Wangali ambaye ndiye chanzo cha kuwekwa sheria hiyo baada ya kusimama kidete kuanzishwa
kwa sheria hiyo, alikuwa akikumbwa na hadha wkt akitaka kumpa chakula mwanaye
mdogo.
Ameongeza
kuwa imefika wakati jamii ielewe kuwa kunyonyesha mtoto mchanga si suala la kuona
aibu hasa unapokuwa eneo lolote ilimradi mtoto akiwa na uhitaji wa
kunyonyeshwa, bali iwe ni jambo la kawaida na kutoa mfano kwa mtu yeyote
anayetaka kula, "inakuwaje pindi unapotaka kula na unafunikwa kichwa?"
Suala la
unyonyeshaji limekuwa ni tatizo kwa miongo kadhaa sasa hususani kwa kizazi cha
sasa kutokana na mazingira yalivyo, vilevile ikiarifiwa kwa kina mama kutakiwa
kunyoshesha watoto kwa takribani miezi sita ya mwanzo mara baada ya kuzaliwa.
pamoja na kupitishwa kwa sheria hiyo bado kuna hoja kwa nini bunge hilo halijaweza kuwa mfano wa kuigwa kwa kuanza kuweka sehemu hiyo?

Post a Comment