Dr. Paulo P. Mhame -Kaimu Mkurugenzi msaidizi Tiba Asili na Tiba Mbadala |
Nchini Tanzania baadhi ya wananchi wamekuwa na elimu ya
matumizi ya dawa za asili inayokana eitha na mazingira au uhusiano wa mtu
anapoishi. Ikiwa ni miaka 13 imepita tangu maadhimisho ya kwanza kufanyika
baada ya mawaziri wa Afya wan chi wanachama wa shirika la Afya duniani kuridhia
kuwepo kwa sherehe hizo.
Nchini Tanzania maadhimisho naya yanafanyika kukiwa na
malengo makuu manne, kwanza Tanzania ina nia ya kufufua ari na kujenga heshima
ya huduma za tiba za asili ambapo historia inatuambia kuwa zilikandamizwa na
kudharauliwa kwa kiwango kikubwa na ukoloni mambo leo, hali inayofanya waafrika
wenyewe wazinyanyapae tiba hizo.
Pili, kupitia maadhimisho haya, serikali inawahamasisha
waganga wa tiba asili kujiepusha na migongano katika jamii kwa kutohusisha
ushirikina na uchawi kama chanzo cha ugonjwa.
Tatu, masuala ya uboreshaji wa dawa asili, aitha utafiti
endelevu wa dawa za asili kwa magonjwa mbalimbali unahimizwa kwa madhumuni ya
kupata dawa ambazo zinaweza kupatikana kiurahisi ili mwenye kuhitaji aweze
kupata.
Nne, kupitia maadhimisho haya waganga wa tiba asili
wanahimizwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma na huduma za
Afya.
Pampja na malengo hayo ujumbe maalum au kauli mbiu iliyobeba
ujumbe kwa mwaka huu “KANUNI ZA UTHIBITI WA BIDHAA ZA TIBA ASILI KATIKA KANDA
YA AFRICA” inawalenga na kutoa majukumu kwa waganga wa Tiba Asili na Mamlaka za
usimamizi katika suala zima la keratibu kanuni na taratibu kusajili na kuthibiti bidhaa zitumiwazo
katika huduma za tiba asili nchini.
Pia waganga wanashauliwa kuzingatia sheria, kanuni na
taratibu zinazowasimamia katika kuhakikisha kuwa bidhaa zitumiwazo katika
huduma zao zinakuwa zimesajiliwa na kujiepusha na matangazo yanayokinzana na
sheria.
Hapa nchini tumebahatika kuwa na mitidawa mingi inayotibu
magonjwa mbalimbali. Ifahamike kuwa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee
na Watoto inatambua tiba asili kuwa ni taaluma rasmi. Hivyo basi basi waganga wote nchini wanapaswa kuweka mabango hovyohovyo barabarani, na katika vyombo vya habari ni lazima yapate kibali cha Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.
Post a Comment