0
Kutoka kushoto ni Rebecca John -Katibu Mkuu, Katikati Dr. Omary Chillo Rais THS

Kamati ya taasisi ya Tanzania Health summit inayaomba mashirika, makampuni, watanzania na wadau mbalimbali wa sector ya Afya kujitokeza na kuunga mkono kikamilifu na kudhamini mkutano mkuu wa siku mbili wenye lengo la kuongeza nguvu za serikali kuboresha Afya za watanzania kupitia kupashana habari na ujuzi, majadiliano na changamoto na kufikia muafaka wenye njia bora zitakazosaidia kuimarisha huduma za Afya hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa taasisi hiyo Dakta Omary Chillo amesema; mkutano huo utafanyika mnamo tarehe 14-15 November 2016 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl Nyerere {JNICC} Jijini Dar Es Salaam.

Na kuongeza kuwa mkutano huo utashirikisha wadau zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwemo watoa watao huduma za afya, manesi, madactari, wafasia, watunga sera, wachumi, watafiti wa magonjwa, wasambazi wa vifaa tiba na dawa, wawekezaji katika sector ya afya na wadau wote wa maendeleo ya afya.

Hata hivyo Dr. Chillo amesema; mkutano wa mwaka wa mwaka huu utahushisha vipengere mbalimbali vikiwemo vikao vya mashauliano vitakavyogusa mada mbalimbali kama maendeleo ya huduma za afya, taarifa kutoka kwa wataalam waliobobea katika nyanja ya afya kuwasiliasha matokeo ya uchunguzi ikiwemo majadiliano katika vikundi pia maonyesho ya huduma na bidhaa kutoka kwa wasambazaji wa huduma za Afya, yakiwemo mashirika ya umma na mashirika binafsi.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari, alipoulizwa kuhusu mgeni rasmi wa mkutano huo, Dr. Chillo amesema; “tunafanya utaratibu kuweza kumualika Mh. John Pombe Magufuri Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa mgeni rasmi siku hiyo

Naye katibu mkuu wa taasisi wa hiyo Bi. Rebecca John amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye kongamani hilo ili waweze kuchangia mawazo yao ili changamoto wanazokutana nazo kwenye afya ziweze kutatulika kwa wataalam kuzisikia moja kwa moja kutoka kwao.




Katika kuendana na siku hiyo Dr, Chillo amesema kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu itakuwa; “majukumu ya taasisi za umma na binafsi katika kufanikisha sera ya huduma za afya kwa wote"




REBECCA JOHN KATIBU MKUU  -"TANZANIA HEALTH SUMMIT"

Post a Comment

 
Top