Rais John Pombe Magufuri akiongea na wataalam waandisi/engineers katika mkutano wao wa mwaka unaofanyika katika Ukumbi la kati Mlimani City.
Katika mkutano huo Rais amegusia nyanja mbalimbali za uchumi ikiwepo suala la waandisi kuijenga nchi kwa kutumia utaalam wao, ikimaanisha jambo lolote linalofanyika katika maendeleo kila sector muhandisi anahitajika.
Katika mkutano huo uliowaunganisha waandisi wote walio sajiliwa katika Board ya Uhandisi nchini zaidi wa 2500 pia waandisi kutoka nchi za jirani kama Kenya na Uganda waliudhulia mkutano huu uliokuwa na kauli mbiu "Nafasi ya Waandisi"ambapo waandisi walimuunga mkono mheshimiwa Rais JPM katika hadhima ya upatikanaji wa madawati na kumkabidhi kiasi cha tshs 100milioni kama mchango wa waandisi.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam ambaye alipata nafasi ya kuongea kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa alitangaza rasmi siku ya October mosi 2016 kuwa siku ya kupanda miti, ikiwa ni kampeni iliyopewa jina la "MTI WANGU" kwa wakazi wote wa mkoa wa Dar Es Salaam.
Aitha alisema nchi haiwezi kufika katika 'nchi ya viwanda' endapo hatupati nafasi ya kujadiri masuala ya maendeleo kufikia hatua ya uchumi wa viwanda. "endapo kutakuwa na mijadara ya wanauchumi, geologist au kila sector kama mainjinia hawa walivyokutana leo na kupanga namna ya kulisukuma gurudumu la maendeleo, hatutaruhusu katika mkoa wetu mh Rais naomba kabisa unisaidie na univumilie, sitaruhusu wazurulaji, wapiga makelele nataka watu wanaokaa na kuweza kujadiri mambo yanayoweza kuleta tija katika Taifa letu.
Vilevile Rais John Pombe Magufuri alipongeza juhudi za mainjinia nchini huku akigusia kuwafahamu vema waandisi kwa kuwa alipata kufanya nao kazi kwa karibu wakati akiwa waziri wa ujenzi ambapo aliweza kukumbusha hapo nyuma mika 1961 nchi ilkuwa na waandisi wawili (2) tu ambapo ni tofauti na sasa wakati kuna waandisi wapatao mia tatu na zaidi.
Aliwataka mainjinia kuunda kampuni zao ili kuweza kushika na kuendeleza nchi huku wakimsaidia mh Rais, pia alisema "...nimeambiwa mtoa mada ni waziri mwenyewe prof. Muhongo, mumueleze
prof. Muhongo japo sasa hivi hayupo, atakapotoa mada aeleze ni namna gani ataweza kuzuia mchanga wetu usisafirishwe kwenda nje"
PICHA YA PAMOJA: ais John Pombe Magufuri waliokaa (katikati) |
Post a Comment